TPPL YATOA OVYO MCHEZO WA NETIBOLI MASHINDANO YA MEI MOSI MOROGORO.
Mchezaji wa timu ya TPPL Gladness Joseph kulia akitafuta mbinu ya kutoa pasi kwa mwenzake huku akizongwa na mchezaji wa Tamisemi Zawadi Mwangosi wakati wa mchezo wa netiboli katika mashindano ya mei Mosi kweenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro na TPPL ilishinda mchezo huo kwa bao 25-20.
TIMU ya Netiboli ya TPPL imeanza kutoa kutoa ovyo kali katika mashindano ya Mei Mosi baada ya kufunga kuwaadhibu akidada wa timu ya Maliasili katika mchezo wa ufungazi wa mashindano hayo uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro kwa vikapu 56-9.
Katika mchezo huo ambao timu ya akinadada wa Maliasili walionekana kuzidi kila idara uliwapa mwanya timu ya TPPL ambayo inamilikiwa na kiwanda cha Tumbaku mjini hapa kutawala kuchezo mchezo huo na kutengeneza nafasi nyingi za kufunga.
Akina dada wa timu ya TPPL ilianza kujihakikishia ushindi kwenye mchezo huo baada ya kumaliza ungwe ya kwanza wakiwa na bao 25 ambayo yalifungwa na Sikutu Mhembe aliyefunga bao10 huku Gladness Joseph akifunga bao 15.
Wakati mabao ya Maliasili katika ungwe hiyo wakifunga jumla ya bao sita na Patrikia Matagi akifunga bao 4 huku Mwanamwisho Kinagi akifunga bao 2.
Katika ngwe ya pili timu ya TPPL iliongeza juhudi kwa kushambulia lango la wapinzani wao na kufanikiwa kufunga mabao 31 kupitia kwa wafungaji wao Sikutu Mhembe akifunga bao 8 huku Gladness Joseph akifunga bao 25.
Huku timu ya Maliasili ikipata mabao matatu katika ngwe hiyo Patrikia Matagi akifunga bao 2 huku Mwanamwisho Kinagi akifunga bao 1.
Katika mchezo mungine timu ya CDA iliweza kuibuka na ushindi wa bao 43-7 dhidi ya Ukaguzi.
0 comments:
Post a Comment