BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MABAO TISA YATINGA MASHINDANO YA TAIFA CUP KITUO CHA MORO.

JUMLA ya mabao tisa yamefungwa katika michezo sita ya mashindano ya Taifa Cup huku kadi 11 zikitolewa kwa wachezaji wa timu nne zilizoshirikisha mashindano hayo yaliyomalizika hivi karibuni katika kituo cha Morogoro kwenye uwanja wa Jamhuri mjni hapa.

Akizungumza na gazeti hili mjini hapa msimamizi mkuu wa mashindano hayo kituo cha Morogoro, Isabellah Kapera alisema jumla ya mabao tisa yamefungwa katika michezo sita na kadi 10 za njano na kadi moja nyekundu zilitolewa.

Kapera alisema kuwa katika mashindano hayo pia kulikuwa na zawadi mbalimbali ambapo mchezaji, Said Salum wa timu ya mkoa wa kisoka wa Ilala alichaguliwa kuwa mchejezaji bora katika mchezo wa ufunguzi kati ya timu yake na wenyeji Moro Stars na hivyo kuibuka na kitita kinono cha Sh100,000 zilizotolewa na mdhamini wa mashindano hayo kampuni ya bia ya TBL.

Wachezaji wengine walioibuka na zawadi ya Sh 100,000 katika michezo mingine baada ya kuchaguliwa kuwa ni ni wachezaji bora wa mechi ni pamoja na, Ally Mohamed wa timu ya Manyara katika mchezo dhidi yake na Moro Stars, Benedict Ngasa wa timu ya Ilala dhidi ya timu ya Pwani.

Wengine ni Seif Rashid wa timu ya Pwani katika mchezo na Manyara kabla ya Modesho Moye aliyeibuka mchezaji bora kwa timu ya Manyara mchezo baina yake na Ilala.

Aidha Kapera alisema kuwa jumla ya kadi 10 za njano zilitolewa na waamuzi wa mashindano hayo baada ya wachezaji kufanya makosa mbalimbali huku mchezaji mmoja, Nicholaus Masiloli wa Manyara akitolewa nje kwa kadi nyekundu kutokana na utovu wa nidhamu kati ya mchezo wa timu yake na Pwani.

Mashindano hayo ambayo yalishirikisha timu nne za mikoa ya Manyara, Pwani, Morogoro na mkoa wa kisoka ya Ilala ya Dar es Salaam ambao ndiyo uliofanikiwa kusonga mbele katika hatua ya robo fainali kutokana na kushinda michezo yake mitatu na kukusanya pointi tisa ikiwa na bao nne ya kufunga na kufungwa bao moja.

Aidha timu ya mkoa wa Morogoro ilikusanya pointi sita na kushika nafasi ya pili ikifunga mabao mbili na kufungwa bao moja wakati timu ya Pwani ilishika nafasi ya tatu na kukusanya pointi tatu, ikifunga mabao matatu na kufungwa bao matatu.

Timu ya mkoa wa Manyara yenyewe ilishika nafasi ya nne ikiwa haina pointi baada ya kupoteza michezo yake yote mitatu na kufungwa bao tatu na kufunga bao moja.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: