wa wahitimu, Willie Shomari mara baada ya kufuzu mafunzo ya ulinzi
ushirikishi jamii kata ya Sabsaba Manispaa ya Morogoro.
HAPA: wakionyesha namna ya kutembea kwa mwendo wa kasi mbele ya mgeni rasmi na wageni waalikwa.
JESHI la polisi mkoani Morogoro limeahidi kukisambaratisha kikosi cha waharifu kinachofahamika kwa jina la ‘mbwa mwitu’ ili kurejesha amani kwa wananchi mjini hapa.
Akizungumza katika hafla ya kufunga mafunzo ya ulinzi shirikishi jamii katika kata ya Sabasaba manispaa ya Morogoro mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai mkoa wa Morogoro, Hamisi Selemani alisema kuwa amepata taarifa ya kuweko kwa kikundi hicho hivyo jeshi limejipanga kukisambaratisha kikosi hicho.
Selemani alidai kuwa kikundi hicho kimekuwa kikifanya uharifu katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Morogoro na limekuwa likidaiwa kujificha katika kata za Mafiga Sabasaba katika mtaa wa Manzese jirani maeneo ya kata ya Sabasaba na Mafiga.
Alisema kuwa baada ya kata hiyo ya Sabasaba kuunda kundi la ulinzi shirikishi jamii litakuwa msaada mkubwa kwa jeshi hilo kutokana na mafanikio yaliyopatikana wakati wa mafunzo hayo ya kuweza kusambaratisha vibaka katika mnada unaofanyika kila jumapili wa Sabasaba.
Mkuu huyo wa upelele alisema pia kuwa jeshi hilo litaweza kukitumia kikundi hicho katika kusambaratisha kikosi cha mbwa mwitu katika kata hizo hususan katika mtaa wa Manzese katika manispaa hiyo.
Katika tukio hilo jumla ya Sh 389,700 na dazani moja ya betri zimepatikana katika harambee ya kuchangia fedha kwa jili ya kukiwezesha kikundi cha ulinzi shirikishi katika kata ya Sabasaba Manispaa ya Morogoro.
Katibu tawala wilaya ya Morogoro, Alfred Shayo aliyekuwa mgeni rasimi katika hafla hiyo alisema fedha hizo zitatumika kukiwezesha kikundi cha ulinzi shirikishi cha kata hiyo kununulia vifaa mbalimbali vya kazi hiyo ya ulinzi.
Shayo alisema kuwa fedha tasilimu Sh 185,000 zilitolewa huku ahadi ikiwa ni Sh 204, 700 ambapo fedha hizo zitatumika kununulia tochi, betri, makoti ya kujikinga na mvua wakati wa doria.
Aidha Shayo aliwataka vijana waliojitokeza katika kazi hiyo kutumia vizuri mafunzo waliyoyapata kwa kufanya kazi ya kulinda amani na mali za wananchi katika kata hiyo.
Katika mafunzo ya ulinzi huo kwa nadhali na vitendo ambapo katika mafunzo ya vitendo yalilenga kuwajengea ukakamavu wa miili na katika utekelezaji wa mafunzo hayo walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa tisa wa makosa mbalimbali na kuwafikisha katika kituo cha polisi.
0 comments:
Post a Comment