

MSHAMBULIAJI WA FARMAGUSTA ABDUL MABOGA AKIMIKI MPIRA DHIDI YA BEKI WA MORO KIDS U23 HAMIS SALEH KATIKA MCHEZO WA MCHEZO WA KWANZA WA MASHINDANO HAYO AMBPO MORO KIDS ILISHINDA KWA BAO 3-1.
TIMU ya soka ya Sabasaba Chipolopolo FC chini ya kiungo wao mahili wa zamani aliyewahi kung’ara na klabu ya Yanga na Moro United Abuu Amlan imepokea kipigo kutoka kwa timu ya Viwawa FC katika mashindano yanayoendelea ya Kamanda Chialo Cup 2011 kwenye uwanja wa Shujaa bao 3-1.
Huku timu ya Maskani nayo itokea kipigo dhidi ya timu ya Mzinga FC kwa kuilaza bao 2-0 yaliyopatikana katika kipindi cha kwanza kwenye mashindano hayo.
Mabao ya washinda yalipatikana kupitia kwa washambuliaji wa timu hiyo ya Maskani Hussei Nassibu kwa adhabu ndogo mpira ulioenda moja kwa moja na bao la pili lilifungwa na Mrisho Ziko katika dakika ya 25 akimalizia mpira uliotemwa na mlinda mlango wa timu ya Mzinga FC Saidi Namchwacha kufutia kombola la Abdul Nassibu kumshinda golikipa huyo na Mzinga FC kupoteza mchezo huo kwa kufungwa bao 2-0.
Sabasaba Chipolopolo FC ambayo ilipwaya katika sehemu ya mlindamlango wao Malidadi Shabaan ilifungwa mabao mawili ya harakaharaka katika dakika ya pili na nne katika kipindi cha kwanza yakifungwa na Hamani Hassani kwa mpira wa adhabu ndogo katika bao la kwanza na bao la pili likifungwa na Salehe Mzee alilofunga akiwa umali wa mita 25 na kwendamoja kwa moja wavuni na kwenda katika mapumziko katika kipindi cha kwanza wakiongoza bao hizo 2-0.
Kiungo huyo alionyesha uwezo mkubwa kwa timu yake kwa kugawa mipira kwa kuttoa pasi kwa washambuliaji wa timu yake lakini safu hiyo ya ushambuliaji ilikosa umakini hasa katika umalizia katika mchezo huo ambao walitawala katika sehemu ya kiungo kwa muda mrefu.
Baada ya kuanza kwa kipindi cha pili timu hiyo ya Sabasaba Chipolopolo ilianza mashambulizi katika lango la Viwawa FC kwa kucheza mchezo wa kasi kwa lengo la kusawazisha mabao hayo lakini safu ya ulinzi ya timu hiyo ya Viwaw FC ilikiwa makini kuondosha hatari zote zilizoelekezwa kwenye lango lao.
Katika mchezo huo timu ya Sabasaba Chipolopolo walipata bao pekee kwa njia ya penalti dakika ya 49 lililofungwa kiufundi na Hussein Golota baada ya mlinzi wa Viwawa FC kufanya madhambi katika eneo la hatari na mwamuzi wa mchezo huo kuamuru ipigwe adhabu hiyo.
Bao la tatu la Viwawa FC lilipatikana katika dakika ya 82 ambalo lilipachikwa wavuni na mshambuliaji wao Justine Makalla na kufanya mchezo kumalizika kwa Sabasaba Chipolopolo kutandikwa kwa bao 3-1.
Katika mchezo mungine timu ya Kaizer Chief ya mjini hapa ilishinda dhidi ya Ulugwai FC kwa kuifunga bao 2-0 yaliyofungwa na Victer Shiwa katika dakika ya 15 na bao la pili likipachikwa wavuni na Gabriel Gabriel na kuibuka na ushindi huo.
katika mchezo wa ufunguzi wa mashindano hayo timu ya soka ya vijana chini ya umri wa miaka 23 ya Moro Kids ilianza vema mashindano hayo kwa kuitandika timu ya Farmagusta katika mchezo uliofanyika uwanja wa Shujaa kwa bao 3-1.
mabao ya washindi yalipatikana katika dakika yamabao mawili yakifungwa na Nahondha wao, Kessi Kidingile aliyefunga dakika ya 49 na 86 bao la kwanza akiunganisha vema krosi ya Ashiri Nassoro na kufunga kwa kichwa wakati bao la pili alifungwa kwa kichwa kufuatia mpira wa kona uliochongwa na Miraji Adamu na kumshinda golikipa wa Farmagusta FC, Joseph Elias na kutinga wavuni na bao la tatu la Moro Kids lilifungwa na Joel Benidict kwa kichwa dakika ya 72 akiunganisha vema krosi iliyopigwa na Ashiri Adam na kuibuka na ushindi huo wa bao 3-1.
wakati bao la kufutia machozi la timu ya Farmagusta lilifungwa na Aman Mazengo katika dakika ya 67.
0 comments:
Post a Comment