BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MAREKANI NA JAPAN KUAMUA NANI BINGWA KOMBE LA DUNIA WANAWAKE 2011 LEO KATIKA ARDHI YA UJERUMANI.


Kushoto ni timu ya wanawake wa Marekani na kulia ni timu ya Japan. Timu hizo zinakumbana katika fainali kesho.

BINGWA WA KOMBE LA DUNIA KATIKA MCHEZO WA SOKA LA WANAWAKE ATAJULIKANA LEO BAADA YA MIAMBA MIWILI MAREKANI NA JAPAN WATAKAPOKIPIGA KUSAKA BINGWA KATIKA MCHEZO WA FAINALI UNAOFANYIOKA LEO JULAI 17 NCHINI UJERUMANI HUKU SWEDEN NA UFARANSA ZIKIWANIA NAFASI YA MSHINDI WA TATU KATIKA MICHUNAO HIYO MIKUBWA.


TIMU ya soka ya wanawake ya Marekani inakabiliana na Japan leo Jumapili wakitafuta ushindi wa tatu wa kombe la dunia, na wakati mbinu na ubunifu zimechukua nafasi ya juu katika mchezo wao na kuwafikisha katika fainali , ni hali ya kujisikia kuwa huru na shauku ambayo timu hiyo inayo, ambayo ndio iliyowaletea mafanikio mara hii katika michezo hiyo hapa Ujerumani.

Katika michezo miwili iliyopita , Marekani iliweza kuzishinda timu mbili, Ufaransa na Brazil , ambapo wachunguzi wengi wa masuala ya soka wanaamini zilikuwa zenye mbinu na wachezaji wenye vipaji kuliko Marekani.

Lakini kocha wa timu hiyo Sundhage alisema ni kutokana na bidii waliyonayo wachezaji wake huku Nahodha wa timu ya Marekani kuhusu mchezo wa fainali wa leo alisema Kucheza katika fainali katika mashindano yoyote ni jambo la kusisimua kila mara ni heshima yenye fadhila kubwa na huwezi kufikia katika kiwango hicho na mchezaji mmoja kichwa kimoja huwezi kufikia hapo kwa mara moja ila kwetu sisi ilikuwa ni juhudi za pamoja kwa kila mtu aliyehusika na sio tu wachezaji lakini hata wasaidizi wetu wote.

Japan nayo imefanikiwa kufikia lengo lao Katika mchezo ya nusu fainali timu hiyo ilipata tena ushindi ilikuwa jinamizi kwa Ujerumani timu ambayo ilikuwa inaota ndoto ya kulitwaa kombe la dunia la wanawake kwa mara ya tatu mfululizo kwa kuichapa bao 1-0 katika dakika za nyongeza lakini pia haikuwapa nafasi Sweden kutamba dimbani Iliipa kipigo cha mbwa mwizi Sweden kwa kuitandika mabao 3-1 huku mashabiki wa Japan wakifurahia ushindi huo walikuwa na haya ya kusema.

"Safi sana walifanya vizuri sana na walikuwa na nafasi nyingi za kufunga lakini tulitumia nafasi tulizopata vizuri".

"Wachezaji wa Japan walicheza vizuri sana, sikutegemea hilo. Wasweden walikuwa ndio wanaotarajiwa kushinda , hata hivyo".

Timu ya mpira wa miguu ya wanawake wa Japan inacheza kwa ajili ya nchi yao na wanaonyesha hivyo kila baada ya mchezo. Kuwa na matumaini ndio nguzo yao kubwa ya kupata motisha.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: