BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MASHINDANO YA KAMANDA CHIALO CUP 2011 HATUA YA PILI.

MSHAMBULIAJI WA TIMU YA DUNDEE FC JUMANNE WIDA KUSHOTO AKIMTOKA BEKI WA ATLAS FC ANDREA MASHAKA.


HAPA MSHAMBULIAJI HUYO, JUMANNE WIDA AKITOKA BEKI WA ATLAS YOHANA SAVEL.


TIMU ya soka ya Dundee FC yenye makao makuu yake kata ya Chamiwno imeendeleza ubabe kwenye mashindano ya Kamanda Chialo Cup 2011 baada ya kuitandika Atlas katika mchezo wa mchunguko wa pili wa mashindano hayo yanayoendelea kwa kuifunga bao 4-0 katika uwanja wa Shujaa mkoani Morogoro.

Mashindano hayo yaliyoandaliwa kwa pamoja na Nyati Sports Promotion na jeshi la polisi mkoa wa Morogoro yenye ujumbe wa ulinzi shirikishi polisi jamii yameanza mzunguko wa pili baada ya timu hiyo ya Dundee FC kufanya vizuri katika mzunguko wa kwanza ambapo ilifamikiwa kuifunga timu ya Uhuru Rangers kwa bao 2-0 huku mchezo wao wa pili dhidi ya Atlas FC ikitoa kipigo kwa mshambuliaji wao hatari wa timu hiyo ya Dundee Jumanne Wida kufunga mabao mawili katika kipindi cha kwanza na cha pili.

Mshambuliaji huyo ambaye ni nahodha alifunga bao lake la kwanza dakika ya nne kipidi cha kwanza kwa kupiga mpira akiwa umbali wa mita 30 na mpira huo kwenda moja kwa moja katika nyavu huku golikipa wa Atlas FC Omari Kizuki asijue la kufanya na kuandika bao la kwanza kwa timu hiyo ya Dundee wakati bao la pili alifunga dakika ya 79 likiwa ni bao la tatu kwa timu hiyo baada ya walinzi wa Atlas FC kuzembea kuondoa mpira katika eneo la hatari na mfungaji kufunga bao hilo.

Mabao mengine ya Dundee FC yalifungwa na Hashim Hamza aliyefunga bao la pili dakika ya 17 kipindi cha kwanza na bao la nne lilihitimishwa na Dismas Anthon aliyefunga kipindi cha pili dakika ya 80 na Dundee kuibuka na ushindi wa bao 4-0 dhidi ya Atlas FC.

Naye Mratibu wa mashindano hayo Shomari Kunguge alisema kuwa jumla ya timu sita zimecheza baada ya kuanza kwa mzunguko wa pili ambapo timu ya vijana ya Moro Kids U23 iliweza kuitandika Viwawa FC kwa bao 2-0.

Alitaja michezo mingine iliyofanyika na matokeo yake kuwa ni Sabasaba Chipolopolo FC ilitoshana nguvu na Kaizer Chief kwa kutoa sare ya bao 1-1 huku Maskani FC ikitoka suluhu ya bila kufungana na Blakc Viba FC wakati Mafisa Lamacia FC ikipoteza mchezo wake dhidi ya Mzinga FC na kutandikwa bao 2-0 na Mindu FC nayo ikipokea kipigo cha bao 3-1 kutoka kwa Assembly.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: