FATUMA KICHINGO AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 10 JELA KWA KOSA LA KUKUTWA NA VIUNGO VYA BINADAMU MORO.
Mkazi wa kijiji cha Wami Dakawa Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro, FatmaKachingo (42) akiwa chini ya ulinzi wa askari polisi huku akiwa na fuvu la binadamu amelishika mikono katika eneo la mahakama ya hakimu mkazi mkoa Morogoro muda mfupi kabla ya kuhukiwa kifungo cha miaka 10 jela kufuatia kukili kosa la kukutwa na viungo vya binadamu kinyume cha sheria mkoani hapa.
FATUMA Kachingo (42) ambaye anadaiwa kuwa ni mganga wa jadi katika kijiji cha Wami Dakawa wilaya ya Mvomero anayedaiwa kukutwa na fuvu pamoja na ngozi ya binadamu amehukumiwa kwenda jela miaka 10 kufuatia kukiri kosa la kukutwa na viungo vya binadamu kinyume cha sheria mkoani Morogoro.
Hukumu hiyo imetolewa na hakimu mkazi wa Mahakama ya mkoa wa Morogoro, NuruPrudencia Nasari baada ya mshitakiwa namba moja ambaye ni mwanamke kukiri shitaka lake huku mumewe akirudishwa mahabusu baada ya kukana shitaka wakati walipofikishwa katika mahakama hiyo kwa mara ya kwanza na kusomewa shitaka hilo wote pamoja.
Hakimu Nasari akisoma hukumi hiyo kwa Fatuma Kichango alisema kuwa kosa alilokutwa nalo mtuhumu la kumiliki viungo vya binadamu ni kinyume cha sheria za nchi hivyo anatoa hukumu ya kwenda jela miaka 10 ili iwe fundisho kwa watu wenye tabia kama hiyo ambapo miaka hiyo inatokana na utetezi wa mshitakiwa kwa kuwa hajawahi kushitakiwa na kosa lolote la jinai na kwamba ana mtoto mdogo anayemtegemea kwani jambo hilo ni la kutisha katika jamii.
Nassar alisema pia mahakama imeona kuwa ni kuwa na vitu kama hivyo na kwamba ametoa adhabu hiyo ili iwe fundisho kwa wengine ambao wanamiliki vitu kama hivyo.
Awali akisoma shitaka, Mwendesha Mashitaka wa polisi Lameck Wabi alidai kuwa washitakiwa hao kwa pamoja walikutwa na Fuvu na ngozi ya binadamu pamoja na vifaa vingine vinavyodhaniwa kuwa vya kishirikiana.
Alivitaja vitu vingine kuwa ni pamoja na magamba ya konokono pamoja na vitu vingine vinavyodhaniwa kuwa vya kishirikina na kwamba vilikutwa chumbani kwa watuhumiwa hao ambao ni mke na mume kwenye nyumba wanayoishi.
Alidai kuwa wahitakiwa hao, walikamatwa Oktoba 29 mwaka huu saa 2 asubuhi katika aneo la Wami Dakawa Wilayani Mvomero, ambapo walipandishwa kizimbani na kusomewa shitaka lao Novemba 1 mwaka huu.
Mwendesha mashitaka huyo aliiomba mahakama itoe adhabu kali kwa mshitakiwa, kwa kuwa kumiliki viungo vya binadamu ni kosa kisheria.
Kwa Upande wake mshitakiwa alipotakiwa kujitetea aliiomba mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa ana mjukuu wake anayemtegemea mwenye umri wa miaka minne ambaye aliachiwa na mtoto wake aliyefariki.
Naye mshitakiwa namba mbili wa shitaka hilo Mogela Victory aliposomewa shitaka lake kwa mara ya kwanza, alikana na kesi yake itatajwa tena Novemba 16 mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment