IAE YAJIPANGA BAADA YA KUSHINDWA KUFANYA VIZURI MASHINDANO YAJAO YA SHIMIVUTA MWAKA 2012/2013.
Mshambuliaji wa timu ya soka ya taasisi ya elimu ya watu wazima Dar es Salaam (IAE), Juma Mdee kushoto akimtoka kiungo wa timu ya chuo cha usimamizi wa fedha (IFM), Edwin Kavishe kulia wakati wa mashindano ya shirikisho la michezo ya vyuo vya elimu ya juu Mchanganyiko Tanzania (SHIMIVUTA) 2011/2012 mchezo uliofanyika uwanja wa Jamhuri Morogoro ambapo katika mchezo huo IFM ilishinda kwa bao 3-0.
BAADA ya kutandikwa mabao 15 katika michezo mitano ya michuano ya shirikisho la michezo ya vyuo vya elimu ya juu mchanganyika Tanzania (SHIMIVUTA) uongozi wa michezo wa taasisi ya elimu ya watu wazima Dar es Salaam (IAE) umeanza kuweka mikakati ya kuandaa timu za michezo mitatu tofauti kwa ajili ya maandalizi ya mashindano yajao ya shirikisho hilo kwa mwaka 2012/2013.
Waziri wa michezo wa taasisi ya elimu ya watu wazima Dar es Salaam,Thomas Aloyce alisema kuwa uongozi wa michezo wa taasisi hiyo umeanza kuweka mikakati mapema kwa kuandaa timu tatu tofauti za michezo ya soka, netiboli, wavu na riadha huku akidai kufanya vibaya kwa timu ya taasisi hiyo.
Aloyce alisema kuwa imetokana na changamoto mbalimbalizi zikiwemo cha ukosefu wa uhaba wa viwanja vya kufanyia mazoezi, ukosefu wa vifaa na kukosa michezo ya kirafiki hali iliyopelekea timu yao ya soka kutandikwa bao 15 katika mashindano hayo ya Shimivuta na kuishia kwenye hatua ya makundi yaliyomalizika hivi karibu katika ardhi ya mkoa wa Morogoro.
Aloyce alisema kuwa kwa sasa uongozi umeanza mchangoto wa kutafuta wachezaji kwa kuanzisha mashindano ya michezo tofauti ndani ya taasisi ili kuweza kupata wachezaji wazuri ambao wataunda timu hizo ambazo zitaendelezwa kwa kupewa michezo mbalimbali ya kirafiki ili mashindano yajao waweze kutoa ushindani mkali wa michezo hiyo hata kutwaa vikombe hivyo.
“tumepoteza michezo mitano dhidi ya wapinzani wetu na kufungwa mabao 15 katika shimivuta ya mwaka huu lakini hii imechangiwa na ugeni wa ushiriki wetu na zikiwemo na chanagamoto nyingine za ukosefu wa vifaa vya michezo, uhaba wa uwanja kufanyia mazoezi pamoja na kukosa michezo ya kujipima nguvu kabla ya kuanza kushiriki mashindano hayo hivyo navyo ni moja ya sababu za sisi kufanya vibaya katika mchezo wa soka” alisema Waziri huyo.
Aloyce alisema katika michezo hiyo mitano waliyocheza dhidi ya wapinzania wao wamefanikiwa kufunga mabao mawili yaliyofungwa na washambuliaji Sadiki Linjenje na Benedict Philipo katika michezo miwili waliyopoteza dhidi ya timu ya taasisi ya teknolojia Dar es Salaam (DIT) na chuo cha Mwalimu Nyerere Kivukoni (MNMA) kwa kufungwa bao 3-1 kila mchezo.
Michezo mingine mitatu waliyopoteza ni pamoja na chuo cha uhasibu Arusha (IAA) kwa kufungwa bao 2-0, chuo cha uhasibu Tanzania (TIA) bao 3-0 na chuo cha usimamizi wa fedha (IFM) bao 3-0.
0 comments:
Post a Comment