BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SHIMIVUTA YATUMIA SH4.9MILI HUKU IKIKUSANYA SH 160,000 KUTOKANA NA ADHABU YA UTOVU WA NIDHAMU.

JUMLA ya sh4.9Mil zimetumika katika michuano ya shirikisho la michezo ya vyuo vya elimu ya juu mchanganyika Tanzania (SHIMIVUTA) huku vyuo viwili vikitozwa faini ya sh160,000 kwa utovu wa nidhani kwa wachezaji wao wakati wa mashindano hayo yaliyomalizika hivi karibuni mkoa wa Morogoro.

Rais wa shirikisho la michezo ya vyuo vya elimu ya juu mchanganyika Tanzania (SHIMIVUTA), Kilomo Matayo alisema kuwa jumla ya sh4.9mil zimetumika katika michuano hiyo ya mwaka huu huku vyuo viwili vya elimu ya biashara (CBE) na chuo cha uhasibu Tanzania (TIA) vikitozwa faini ya kiasi cha sh 160,000 kila chuo kutokana na utovu wa nidhamu ulionyeshwa na wachezaji wake wakati wa mashindano hayo.

Matayo alisema kuwa chuo cha CBE ndicho kilichoibuka kuwa kinara wa utovu wa nidhamu baada ya kamati ya nidhamu kukikuta na makosa mawili, moja likiwa la mchezaji wake kutimuliwa katika mashindano hayo kutokana na kudaiwa kufanya fujo wakati timu ya netiboli ya chuo hicho ikicheza huku mungine akipatikana na madai ya kufanya vurugu wakati timu ya soka ikicheza na moja ya wapinzani wao uwanja wa jamhuri na kutozwa kiasi cha faini sh 80,000 kutokana na makosa hayo.

Aidha chuo cha TIA nacho kilitozwa faini ya sh 80,000 kutokana na madai ya mmoja wa wacheziji wake kudaiwa kufanya fujo ambapo kamati hiyo ilitoa adhabu kila chuo na kufanya kamati hiyo ya shimivuta kujipatia kipato baada ya kukusanya kiasi cha sh 160,000 huku kikitumia kiasi cha sh 4.9mil katika mashindano hayo. Alisema Rais huyo.

Matayo alisema kuwa kiasi cha sh4.9mili zilitumizi katika shughuli mbalimbali zikiwemo za utawala, kulipa waamuzi waliochezesha michezo yote kuanzia hatua ya makundi, nusu fainali na fainali, malazi kwa viongozi wa shimivuta na ghalama za kukodi viwanja vya michezo mitano ya soka, netiboli, kikapu, wavu na riadha iliyofanyika viwanja vitatu tofauti vya chuo cha ujenzi Morogoro, Bwalo la Umwema JKT na Jamhuri na kufanya ghalama zote kufikia sh 4.9mil.

Kwa upande wa zawadi za washindi wa kwanza, pili na tatu zawadi za vikombe kwa michezo yote mitano ikitolewa na tawi la kampuni ya simu za mkononi ya tecno la jijini Dar es Salaam kukipongeza chuo cha elimu ya biashara (CBE) kwa kutwaa makombe matatu ya soka, netiboli na kikapu huku akitoa wito kwa viongozi mbalimbali wanaoshiriki michuano hiyo kuwa karibu na wachezaji wao pindi timu zinapocheza na wapinzani kwani hilo litasaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa utovu wa nidhamu kutokana na uwepo wao viwanjani. alisema Rais huyo wa Shimivuta.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: