SERIKALI YATENGA SH15.4BIL ILI KUBORESHA MIUMNDOMBINU YA ZAO LA MIWA NCHINI.
Mkurugenzi wa sheria na udhiti bodi ya sukari Tanzania, Henry Semwaza akifafanua jambo wakati wa warsha kuhusu mikakati ya wakulima wa miwa na maendeleo ya nishati mimea mbadala na upungunzaji wa umasikini iliyofanyika hivi karibuni mkoani Morogoro.
ILI kukabiliana na upungufu wa tani 500,000 za sukari zinazohitaji kwa mwaka serikali imetenga kiasi cha sh15.4milioni kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya zao la miwa nchini.
Akizungumza katika mahojiano maalum na gazeti hili mjini Morogoro Mkurugenzi wa sheria na udhibiti bodi ya sukari Tanzania, Henry Semwaza alisema serikali imetenga kiasi hicho kwa ajili kuboresha miundombinu ya zao la sukari ili kuweza kufikia kiwango cha tani 500,000 za surika ambazo zinahitajika kwa mwaka.
Semwaza alisema kuwa kwa sasa Tanzania inazalisha tani 300,000 za sukari kwa mwaka wakati mahitaji yake ni tani 500,000 kwa mwaka hivyo mpango huu utakapomalizika utapunguza kwa kiasi tatizo la upungufu wa sukari.
Katika mpango huo wa kuboresha miundombinu unakwenda sambasamba na mpango wa kuanzisha viwanda vidogo vidogo vya kusindika sukari kwa lengo la kupunguza tatizo la upungufu wa sukari kwa mwaka na kukidhi matumizi ya ndani mpango ambao utaonza mwaka 2012/2014.
Semwaza alisema kuwa fedha hizo zitaelekezwa katika mashamba ya Mtibwa na Kilombero mkoani Morogoro na mkoa wa Kagera ambapo itaendeleza miundombinu ya wakulima wa zao la miwa ikiwemo umwagiliaji.
“Serikali imetenga kiasi cha sh15.4Bil katika awamu ya pili kwa ajili ya kukabiliana na upungufu wa tani 500,000 za sukari ambazo zinahitaji kwa mwaka lengo likiwa ni pamoja na kuendeleza na kuboresha miundombinu ya zao la miwa nchini,” alisema Semwaza.
Kuboresha kwa miundombinu hiyo kutachangia sana ongezeko la uzalishaji wa zao hilo na hivyo kuweza kukidhi mahitaji ya ndani na ziada kuuza nje, wakati huo huo kutapunguza uagizaji wa bidhaa hiyo kutoka nje ya nchi.
0 comments:
Post a Comment