Juma Mtanda akishiriki kazi za kijamii kwa kufanya usafi wa mazingira katika mfereji unaopita katika mtaa wa Sina kata ya Mafisa Manispaa ya Morogoro ili kukabiliana na changamoto za maji kuingia katika makazi ya watu inayosababisha na mfereji huo kujaa uchafu na maji kushindwa kupitika katika mkondo wake.
Mwenyekiti wa mtaa wa Sina kata ya Mafisa Manispaa ya Morogoro, John Sweya, kushoto akishirikiana na wananchi wa mtaa wa Sina kufanya usafi wa mazingira kwa kusafisha mfereji unaopita eneo hilo ambapo usafi huo utasaidia kupunguza kero ya maji kwenda katika makazi ya watu kutokana na mfereji huo kujaa uchafu mkoani hapa.
Sehemu ya wananchi wakishiriki usafi wa mazingira kwa kuondoa uchafu ndani ya mfereji unaopita eneo hilo.
Mwenyekiti wa mtaa wa Sina kata ya Mafisa Manispaa ya Morogoro, John Sweya, kushoto akishirikiana na wananchi wa mtaa wa Sina kufanya usafi wa mazingira kwa kusafisha mfereji unaopita eneo hilo ambapo usafi huo utasaidia kupunguza kero ya maji kwenda katika makazi ya watu kutokana na mfereji huo kujaa uchafu mkoani hapa.
WAKAZI wa mtaa wa Sina kata ya Mafisa Manispaa ya Morogoro wameanza kutekeleza maadhimio ya mkutano wao wa kuondoa baadhi za kero ikiwa ni pamoja na kuziba kingo za mto Morogoro na kufanya usafi wa mfereji inayopita unaopita katikati ya mtaa huo kujinusuru na mafuriko.
Akizungumza na gazeti hili mkoani hapa Mwenyekiti wa mtaa huo, John Sweya alisema wakazi 73 wamejitokeza kufanya usafi wa mazingira kwa kusafisha moja ya mirefeji inayopita katikati ya mtaa huo ili kukabiliana na maji ambayo yanahofiwa kuweza kuvamia makazi yao kutokana na mifereji ya maji kujaa uchafu.
Sweya alisema kuwa maadhimio yaliyofikiwa na mkutano huo wa hadhala uliofanyika hivi karibuni ni pamoja na ajenda ya sheria ndogo ya faini ya sh20,000 kwa mkazi ambaye hataweza kufika katika kazi ya kujitolea kulekebisha mifereji hiyo na ile ya barabara kuu ya Msamvu - Kayenzi.
“Maadhimio ya mkutano wetu yameanza kuzaa matunda baada ya wananchi 73 kujitokeza katika kampeni ya kupunguza baadhi ya kero katika mtaa wetu ikiwemo kufanya usafi wa mazingira kwa kusafisha moja ya mrefeji unaopita katikati ya mtaa ambapo umekuwa kero wakati wa masika,” alisema Sweya.
Aidha mwenyekiti huyo alisema kuwa katika siku ya kwanza wakazi 17 walitajwa kutoshiriki kufanya usafi hivyo kwa mujibu wa sheria ndogo za mtaa huo watatozwa faini ya Sh20,000 na ikiwa watakaidi watafikishwa mahakamani.
Naye mkazi wa mtaa huo, Hamis Kandi alisema kuwa ipo haja kwa Mwenyekiti wao kuwa makini katika usimamizi wa agenda za mkutano zilizoadhimiwa na wakazi hao kwani kumekuwa na baadhi ya wananchi kuupuuza maadhimio ya mikutano.
Kandi alisema kuwa mwenyekiti anapaswa kusimamia kikamilifu maadhimio na kuwachukulia hatua kama walivyokubaliana katika mkutano ili siku nyingine maadhimio yanayopitishwa katika mkutano yatekelezwe kwa asilimia 100.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / Uncategories / WAKAZI WA MTAA WA SINA MORO WAANZA KUTEKELEZA MAADHIMIO YA MKUTANO KWA KUONDOA BAADHI YA KERO KUONDOKANA NA MAFURIKO.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment