BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MEYA AWATAKA WAAJIRI KUIPA MICHEZO KIPAUMBELE


MSTAHIKI MEYA WA MANISPAA YA MOROGORO AMIR JUMA NONDO.

Na Venance George, Morogoro

MEYA wa Manispaa ya Morogoro, Amir Nondo, amewataka viongozi na waajiri katika idara na wizara za serikali kulipa kipaumbele suala la michezo kwa wafanyakazi wake ili kulinda
afya na kuimarisha mahusiano kwa watumishi wa umma.

Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo maalum kwa makatibu, wenyeviti na maafisa michezo kutoka idara na wizara za serikali yaliyoandaliwa na Shirikisho la Michezo
katika Idara na Wizara za Serikali (SHIMIWI), Nondo alisema kuwa licha ya
serikali kuona umuhimu wa michezo kwa watumishi wa umma bado wako viongozi
wanaokwamisha dhamira hiyo.

Nondo alisema kuwa michezo mbali ya kusaidia kuimarisha afya za wafanyakazi, lakini bado
hujenga mahusiano miongoni mwao na hivyo kuimarisha utendaji kazi na kufikia malengo ya maendeleo ya taifa.

Kwa upande wake katibu mkuu wa Shimiwi, Ramadhan Sululu, alisema kuwa mafunzo hayo ni
muendelezo wa mafunzo yanayotolewa na shirikisho hilo katika kuwajengea uelewa
viongozi na wanamichezo juu kanuni na sheria za michezo mbalimbali.

Sululu alisema kuwa katika mafunzo hayo kwa wenyeviti, makatibu na maafisa wa michezo katika idara na wizara za serikali ya siku tano yanayolenga kuwawezesha kujua katiba,
majukumu na wajibu wa kila kiongozi katika michezo.

Hata hivyo, Sululu alisisitiza kuwa Shimiwa inakusudia kukutana na makatibu wakuu wizara ya
utumishi wa umma na wizara ya habari, vijana, utamaduni na michezo ili kujadili
juu ya idara na wizara zinazopuuza suala la michezo katika maeneo yao ya kazi.

Alisema kushindwa kushiriki kwa baadhi ya wanachama katika mafunzo hayo na mashindano
yanayoandaliwa na Shimiwi kila mwaka si kwa tatizo la ukosefu wa fedha badala
yake ni kukosa hamasa kwa viongozi hao.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: