Na Mwandishi wetu morogoro
TIMU ya soka ya wachezaji wa zamani wa mkoa wa Morogoro” Morogoro veterans” inataraji kucheza michezo miwili ya kirafiki mkoani Dodoma jumamosi hii.
Michezo hiyo miwili itakuwa ni dhidi ya timu ya wachezaji wa zamani wa mkoa wa Dodoma”Dodoma Veterans ambayo itapigwa katika uwanja wa jamhuri mjini Dodoma.
Katibu mkuu wa timu ya Morogoro veteran Abubakari Fungo amesema kuwa mchezo wa kwanza utapigwa jumamosi hii majira ya saa 10. 30 jioni na mchezo wa pili utapigwa kuanzia saa mbili asubuhi katika uwanja huo huo wa jamhuri.
Tayari makocha wa timu zote mbili wameanza kutambiana kuibuka na ushindi katika
michezo hiyo,kocha mkuu wa Morogoro veteran Amri Ibrahimu alisema kuwa kipigo hakikwepeki kwa Dodoma Veterani wakati ambapo Charles Mgodo wa Dodoma veteran akisema kuwa watashinda kwa mabao mengi.
Morogoro veteran inategemea kuwatumia boniphace Njohole,mchawi Mbeta, Profesa Madundo mtambo,Abdalllah kondo, Godfrey Kikumbizi na Salhina Mjengwa kusaka ushindi huo wakati ambapo Dodoma veteran ikitaraji kuwatumia akina Issa Kihange, Bahati Masangija na Henry Mkanwa kuwakabili Morogoro veteran.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment