BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

POLISI MORO KATIKA KASHIFA NYINGINE


Na Venance George, Morogoro
JESHI la polisi mkoni Morogoro kwa mara nyingine tena limeingia katika kashfa nyingine baada ya askari wake watatu kutuhumiwa kuiba simu tatu za kiganjani zenye thamani ya zaidi ya Sh 250,000 wakiwa katika harakati za kumkamata mtuhumiwa aliyekuwa amepanga katika nyumba ya kulala wageni iliyoko mtaa wa Sultan Area, manispaa ya Morogoro.

Tukio hilo ambalo limeripotiwa katika kituo kikuu cha polisi mjini Morogoro February 28, mwaka huu kwa RB namba MOR/RB/2450/2012 na kufunguliwa jalada la uchunguzi lilitokea Februari 26 majira ya saa 5.00 asubuhi ambapo askari hao watatu walifika katika nyumba hiyo ya kulala wajeni inayojulikana kwa jina la Geita Guest House wakimtafuta mtu aliyedaiwa kumwibia mwajili wake na kutoweka kisha kujificha katika nyumba hiyo.

Akizungumza na gazeti hili msimamizi wa nyumba hiyo ya kulala wageni, Innocent Mhangirwa alisema kuwa polisi waliofika katika tukio pia waliambatana na msichana mmoja anayedaiwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mtuhumiwa waliyekuwa wakimtafuta.

Mhangilwa alisema kuwa askari hao walimweleza msimamizi wa nyumba hiyo ya kulala wageni kuwa wanamtafuta mtu ambaye anamahusiano na msichana waliyekuwa naye na baada ya kuoneshwa chmba ambao mtuhumiwa huyo alikuwa walijaribu kuufungua na kubaini kuwa ulikuwa umefungwa kwa ndani.

“Baadaye niliwataka askari hao kuwa wavumilivu ili nikachukue funguo za akiba za chumba hicho ili tujaribu kuufungua lakini cha ajabu wakati nakwenda chumba nilishangaa kuona askari wawili kati ya wale watatu walikuwa wakinifuata nyuma mpaka nilipoingia chumbani na kuuchukua ufunguo huo,” alisema Mhangirwa.

Aliongeza kuwa wakati zoezi la kuchukua funguo likiendelea mmoja wa akari hao aliingia sebureni na kisha kutoka haikujulikana mara moja alikwenda kufuata nini lakini baada ya askari
hao kufanikiwa kufungua mlango na kumtia mbaroni mtuhumiwa waliyekuwa wakimtafuta ambaye katika kitabu cha kulala wageni alijiandikisha kwa jina la Joseph Shamba, ndipo walipogundua kuwa simu zao tatu zimeibiwa.

“Baada ya askari kuondoka mimi nilikwenda sebuleni nilikokuwa nimeweka simu zangu lakini cha kushangaza si simu zangu wala simu ya kaka iliyokuweko sebuleni huko,” alisema msimamizi mwingine wa nyumba hiyo ya kulala wageni aliyejitambulisha kwa jina la Michael
Mhangirwa.

Aliongeza kuwa baada ya kubaini kutokupo kwa simu hizo walijaribu kutumia simu ya mtu mwingine kupiga lakini hakuna simu kati ya zile tatu iliyopatikana na kulazimika kuwenda kituo kikuu cha polisi kutoa taarifa juu ya tukio hilo.

Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro, Adolfina Chialo, alipohojiwa juu ya tukio hilo alisema kuwa hana taarifa zozote juu ya tukio hilo lakini alisisitiza kuwa askari polisi kama binadamu wengine anaweza kushikwa na tamaa na kushiriki katika tukio hilo.

“Mimi siwezi kukataa moja kwa moja kuwa askari hawakuiba simu hizo, lakini ninachojua ni kwamba polisi kama binadamu anaweza kughafilika na kujikuta akishiriki katika uharifu, lakini
nawaomba hao vijana walioibiwa simu zao wafungue jalada ili kulifanyie uchunguzi,” alisisitiza.

Hata hivyo habari zailizopatikana siku mbili baada ya jalada la upelelezi kufunguliwa mmoja wa askari aliye daiwa kushiriki katika tukio hilo alirudi katika nyumba hiyo ya kulala wageni akitaka kufanya mazungumzo na wasimamizi wa nyumba hiyo lakini hata hivyo hakufanikiwa kukutana nao.

Hivi karibuni baadhi ya askari polisi wa kituo cha polisi cha Dakawa wilayani Mvomero mkoani Morogoro walituhumiwa kumpiga mlemavu wa akili na viungo na kulazimika kupelekwa hospitali ya muhimbili kwa matibabu zaidi baada ya kupata rufaa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro, Mlemavu huyo alidaiwa kuiba sufulia tupu.



Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: