Meya wa Manispaa ya Morogoro, Amir Juma Nondo wa pili kushoto akimkabidhi mfano wa hundi Meneja uendeshaji kampuni ya Jae-Hi-Teach Dary Cleaning Maximillian Makota kwa ajili ya uchimbaji wa visima kwa shule za sekondari 12 za Manispaa hiyo ya sh26.7Mil hafla iliyofanyika ukumbi wa Manispaa hiyo kulia ni Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL, Steven Kilindo na kushoto ni Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Jovis Sembeyi.
Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL, Steven Kilindo aifafanua jambo wakati wa utoaji wa hudni kwa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Jovis Sembeyi, Meneja uendeshaji kampuni ya Jae-Hi-Teach Dary Cleaning Maximillian Makota na kulia ni Meya wa Manispaa ya Morogoro Amir Juma Nondo.
Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL, Steven Kilindo kulia akikabidhi hundi kwa DK Ntoli Mwakibete ambaye ni Kaimu Mganga Mfawidhi hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro yenye thamani ya sh24.9Mil kwa ajili ya kuchimba kisima kitakachosaidia kupunguza kero ya maji katika hospitali hiyo.
Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL, Steven Kilindo kulia akizungumza jambo kabla ya kukabidhi hundi hiyo na kushoto ni Afisa Ustawi wa JamiiSekretarieti ya mkoa wa Morogoro Tabitha Matiku
SEHEMU YA WAFANYAKAZI WA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA HUO.
SHULE 12 za sekondari zilizoko katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro na hospitali ya mkoa, zimepeta msaada wa Sh51.6 kwa ajili ya kuziwezesha kuchimba visima, kuweka matangi ya kuhifadhia maji na dawa katika shule hizo.
Fedha hizo zimetolewa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) chini ya mkakati wake wa kuboresha huduma za maji katika taasisi mbalimbali.
Akikabidhi fedha hizo juzi, Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL, Steven Kilindo, alisema Sh24.9 milioni katika fedha hizo ni kwa ajili ya hospitali ya Mkoa wa Morogoro.
Alisema kampuni hiyo imekuwa ikitumia sehemu ya pato lake, kuiwezesha jamii kuondokana na kero ya kukosa huduma za maji.
Akizungumza kwa niaba ya uongozi wa hospitali ya mkoani hapa, Kaimu Mganga Mkuu, Ntobi Mwakibete, alisema fedha hizo zitasaidia kupunguza kwa kiwango kikubwa tatizo la maji katika hospitali hiyo.
“Hapa hospitalini kuna wakati tulikabiliwa na tatizo la maji kwa takribani siku mbili. Kwa kweli ilikuwa ni shida kubwa kwa sababu maji yanahitajika wakati wote katika uendeshaji wa shughuli za hospitali,”alisema Mwakibete.
Ofisa Afya wa Mkoa wa Morogoro, Carl Lyimo, alisisitizia umuhimu wa kuchimba visima katika maeneo salama ili maji yatakayopatikana yaweze salama na kwa matumizi ya wagonjwa na shughuli nyingine za hospitali.
Kampuni ya Bia Tanzania pia ilikabidhi Sh26.7 milioni kwa uongozi wa Manispaa ya Morogoro, ili kugharimia uwekaji wa matangi ya maji na dawa katika shule 12 za sekondari ya manispaa hiyo.
Shule zitakazonufaika na msaada huo ni Bondwa, Bungodimwe, Kingo, Kola Hill, Mjimpya, Mgulasi, Uluguru, Uhuru, Nanenane, Tubuyu, Mafisa na Tushikamane ambazo ni shule za kata.
Meya wa Manispaa ya Morogoro, Amir Nondo, alisema msaada huo ni muhimu hasa ikizingatiwa kuwa shule nyingi katika Manispaa ya Morogoro, hazina huduma za maji.
Nondo alisema hata hivyo manispaa imekuwa ikijitahidi kuboresha huduma za maji na kwamba hivi karibuni, imepima viwanja katika maeneo ya Kiegeya A na B, Kipera, Kasanga na Mbunge kwa ajili ya uchimbaji wa visima virefu.
0 comments:
Post a Comment