
Mlinzi wa Uhuru Rangers, Fadhil Seleman kulia akiwania mpira dhidi ya mshambuliaji wa timu ya soka ya Mkamba Rangers Fadhali Pangapnga kushoto wakati wa mchezo wa fainali wa ligi ya taifa kuwania ubingwa wa mkoa wa Morogoro 2011/2011 katika uwanja wa Jamhuri mkoani hapa ambapo mchezo huo ulimalizika kwa sare ya bao 1-1.

Mshambuliaji wa timu ya soka ya Mkamba Rangers Waziri Ramadhan kulia akichuana na mchezaji wa Uhuru Rangers, Salum Matete wakati wa mchezo wa fainali wa ligi ya taifa kuwania ubingwa wa mkoa wa Morogoro 2011/2011 katika uwanja wa Jamhuri mkoani hapa ambapo mchezo huo ulimalizika kwa sare ya bao 1-1.
MWAMUZI wa kati, Hamis Kambi amelazimikakuvunja mchezo baina ya klabu ya soka ya Uhuru Rangers FC dhidi ya MkambaRangers FC baada ya mlinzi wa klabu ya Uhuru Rangers kumtwanga kichwa mwamuziwa pembeni katika mfululizo wa michezo ya fainali ya ligi ya taifa kuwaniaubingwa wa mkoa wa Morogoro 2011/2012 uliofanyika uwanja wa Jamhuri mkoanihapa.
Mchezo huo ambao ulivunjika dakikaya 80 baada wachezaji wa Uhuru Rangers kupinga maamuzi ya bao la kusawazisha laMkamba Rangers walilofungwa dakika ya 72 na mshambuliaji, Stanlaussy Mkachage kwamadai ya mfungaji aliotea kabla ya kupachika bao hilo na kuzua tafraniiliyodumu kwa dakika nane kabla ya mwamuzi huyo kumaliza mchezo huo ambao ulimalizikakwa sare ya bao 1-1.
Mkamba Rangers ndiyo walioanza kufungwabao katika dakika ya 14 na Uhuru Rangers kupitia kwa mshambuliaji wake, AthumanAlly na kwenda mapumziki wakiongoza kwa bao 1-0 ambapo kipindi cha pili MkambaRangers walisawazisha kwa mpira wa adhabu ndogo nje kidogo ya eneo la hatari ambapompira huo ulimkuta mfungaji ambaye alivunja mtego wa kuotea na kukwamisha mpirakimiani na kufanya matokeo kuwa bao 1-1.
Wachezaji wa Uhuru Rangers baada yakufungwa kwa bao hilo walimfuata mshika kibendela namba mbili, Vicent Bathazaliambapo katika vurugu hizo alitumia nafasi hiyo mlinzi wa Uhuru Rangers, JosephVitus kumtwanga kichwa mwamuzi huyo kwa madai ya kukubali bao kwa madaimfungaji alikuwa ameotea na mwamuzi wa mchezo huo Hamis Kambi kumuonyesha kadinyekundi dakika ya 73.
Mwamuzi huyo kabla ya kumuonyesha kadinyekundu kwa mchezaji wa Uhuru Rangers tayarimwamuzi huyo alimuonyesha kadi nyekundu kwa mchezaji wa Mkamba Rangers, RajabuMrangali dakika ya 63 baada ya kupewa kadi ya njano kutokana na kupingana namaamuzi ya mwamuzi.
Katika mchezo mungine aliofanyikamajira saa 8 mchana Mpepo FC ilifanikiwa kuilaza The Wailes kwa bao 1-0 katikamchezo mkali na wenye ushindani ambapo bao pekee lilipachika nyavuni namshambuliaji, Abas Athmani dakika ya 52.
0 comments:
Post a Comment