
Mchezaji wa klabu ya Mpepo FC, Waziri Mustafa kushoto akiwania mpira dhidi ya mchezaji wa Mkamba Rangers FC Joseph Popoo wakati wa fainali ya ligi ya taifa kuwania ubingwa wa mkoa wa Morogoro ambapo Mkamba Rangers FC waliitwaa ubingwa huo kwenye mchezo wa mwisho uliomalizika kwa sare ya bao 1-1 kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani hapa.
JUMLA ya bao 20 yamepachikwa wavuni katika fainali ya ligi ya taifa kuwania ubingwa wa mkoa wa Morogoro 2011/2012 yaliyoanza kutimua vumbi februari 25 na kumalizika marchi 03 kwa klabu ya Mkamba Rangers FC kutwaa ubingwa wa mkoa huo kwa msimu huu yaliyofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani hapa.
Katika fainali hizo zilishirikisha klabu sita za Mpepo FC, Kaizer Chief FC, Uhuru Rangers FC, Docks FC, Wailes FC na The Mkamba Rangers ambazo zilifuzu kutoka kwenye vituo vya mji mdogo wa Mkamba wilayani Kilombero na wilaya ya Kilosa huku kila kituo kikitoa timu tatu mshindi wa kwanza hadi wa tatu na kushiriki kunyang’anyaro cha kuwania ubingwa wa mkoa wa Morogoro 2011/2012.
Washambuliaji Abdallah Zungu wa klabu ya Mpepo FC na Twaha Mohamed na Asil Elias wa klabu ya Kaizer Chief ndiyo wanaongoza kwa kupachika mabao huku kila mmoja akiwa amevumania nyavu mara tatu katika fainali ya ligi hiyo ambayo ilikuwa na ushinda wa hali ya juu hali iliyopelekea bingwa kupatikana kwa tofauti ya bao moja.
Fainali ya ligi hiyo ilichezwa kwa jumla ya michezo 15 ambapo michezo 10 ilimalizika kwa timu husika kuondoka na ushindi huku sare ya bao zikiwa tatu na sare tasa zenyewe ni mbili ambapo timu ambayo iliibuka na ushindi mkubwa ni Kaizer Chief dhidi ya Docks FC kwa kupchikwa bao 3-0.
Mabingwa wa soka Manispaa ya Morogoro 2011/2012 klabu ya Uhuru Rangers ndiyo iliyofungwa mabao mengi zaidi katika fainali hizo kwa kuruhusu mabao saba huku Docks FC ikitandikwa mabao matano ulikinganisha na timu nyingine wakati katika mabao ya kufunga Mpepo FC ikiwa imefunga mabao saba na Mkamba Rangers FC ikiwa imepachika maba sita.
Jumla ya kadi 17 ziliztolewa kwa wachezaji ambao walionyesha utovu wa nidhamu mchezoni huku kadi nyekundu zikiwa zimetolewa katika mchezo kati ya Uhuru Rangers FC na Mkamba Rangers FC ambapo katika mchezaji wa Uhuru Rangers FC, Joseph Vitus alionyeshwa kadi nyekundi baada ya kumtwanga kichwa mwamuzi msaidizi huku mchezaji Mkamba Rangers, Rajabu Mrangali alionyeshwa kadi nyekundu baada ya kupewa kadi mbili.
0 comments:
Post a Comment