BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

POLISI MORO SC YAJIHAKIKISHIA KUCHEZA LIGI KUU YA VODACOM MSIMU UJAO BAADA YA KUITANDIKA RHINO RANGERS BAO 2-1 LIGI DARAJA LA KWANZA HATUA YA 9 BORA JAMHURI MOROGORO.


WACHEZAJI WA POLISI MORO SC WAKIWA WAMEMBEBA KOCHA MSAIDI JOHN TAMBA MARA BAADA YA KUITANDIKA RHINO RANGERS KWA BAO 2-1 KATIKA MCHEZO WA LIGI DARAJA LA KWANZA HATUA YA TISA BORA NA KUJIHAKIKISHIA KUCHEZA LIGI KUU YA VODACOM MSIMU UJAO.


KLABU ya soka ya Polisi Moro SC imefakiwa kupata moja ya nafasi kati ya tatu za juu za kucheza ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara katika msimu wa mwaka 2012/2013 baada ya kuitandika Rhino Rangers katika mchezo mkali na kusimumua katika mfululizo wa michezo ya ligi daraja la kwanza hatua ya tisa bora yanayoendelea kufanika kwenye uwanja wa jamhuri kwa bao 2-1.


 
katika mchezo huo ambao ulikuwa na ushindani wa hali ya juu kutokana na Polisi Moro SC kutaka kushinda na kujihakikia moja ya nafasi moya kucheza ligi kuu msimu ujao na Rhino Rangers nao wakihitaji kupata ushinda ili nao wapate kujiongezea pointi kufikisha pointi 11 katika michezo saba iliyocheza kwa lengo la kusaka nafasi mojawapo ambapo waaliandika bao pekee kwa kuzifumania nyavu za wapinzani wao kupitia mshambuliaji Abasi Abdallah kufunga dakika ya 65 baada ya safu ya ushambuliaji kushiriana vizuri eneo la hatari na kufunga bao hilo huku mlinda mlango Salum Konda wa Polisi Moro SC asijue la kufanya.
 
Baada ya Polisi Moro SC kutandikwa bao hilo vijana hao wanaonolewa na kocha mkuu John Simkoko walicharuka na kusakata soka la uhakika kwa kufanya mashambulizi ya nguvu lango la wapinzani wao na katika dakika ya mshambuliaji Nicolaus Kabipe alifanyiwa madhambi eneo la hatari na mwamuzi wa mchezo huo Allanus Luwena aliamuru ipigwe adhabu ya penalti iliyopigwa na, Iman Mapunda ambapo mpira huo uligongwa nguzi na kurudi ndani na kumkuta, Ally Shomari aliyetoa pasi kwa Mapunda na kukwamisha mpira kimiani kwa shuti akiwa ndani ya 18 na kujaa wavuni kuandika bao la kusawazisha.

 
Polisi Moro waliendelea kulisakama lango la wapinzani wao na katika dakika 90 mshambuliaji Juma Laizio aliihakikishia Polisi Moro SC kucheza ligi kuu msimu ujao baada ya kufunga bao la pili na ushindi kwa shuti la juu akiunganisha krosi ya Ally Shomari na kumshinda mlinda mlango wa Rhino Rangers, Abdulsalum Mtumwa na kuamusha shangwe kwa mashaabiki wa klabu hiyo.
 
Hali ya mchezo ilibadilika kwa pande zote mbinu huku wachezaji wa pande mbili wakichezeana rafu za makusudi hali iliyopolekea mchezaji wa Rhino Rangers Salum Tabay kuzawadiwa kadi nyekundu na mwamuzi wa mchezo huo Allanus Luwena kutoka Mwanza katika dakika ya 93 na mpira huo kumalizika kwa Polisi Moro kuibuka na ushinda wa bao 2-1mchezo uliofanyika majira ya saa 8 mchana kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro.

 
Katika mchezo baina ya Mbeya City dhidi ya JKT Mlale ulimalizika kwaMbeya City kuibuka na ushindi wa bao 2-1 katika mchezo mkali ambao nao ulikuwa na ushindaji wa hali ya juu huku Mbeya City ikifufua matumaini mapya ya kusaka pointi tatu muhimu ambapo kwa sasa imekusanya pointi nane katika michezo sita iliyocheza.

 
Mbeya City FC iliyopo chini ya kocha mkuu Juma Mwambusi ndiyo ilianza kufungwa na JKT Mlale baada ya mshambuliaji wao tegemeo Immanuel Soda kufumania nyavu katikam dakika ya 35 akiunganisha krosi ya Ismail Kisuke na kuandika bao hilo huku Mbeya City FC walisawazisha kupitia kwa Hassan Mwasapili akiunganisha vema mpira wa adhabu nje ya 18 na kumkuta mfungua aliyefunga bao kiufundi likimwacha golikipa Vita Manyika asijue la mkufanya na mpira kutinga katika nyavu.

 
Wachezaji wao wa Mbeya City FC walilisakama lango la wapinzania wao na dakika ya 73 Baraka Haule aliikosesha timu yake bao la pili baada ya mkwaju wake wa penalti kugonga mwamba wa juu kisha mpira kurudi uwanjani na kuokolewa na walinzi wa JKT Mlale baada ya mlinzi wao kufanya madhambi eneo la hatari.

 
Katika dakika tatu za nyongeza mlinzi wa JKT Mlale Beno Kisewa alinawa mpira katika eneo la hatari na mwamuzi wa mchezo huo Maalim Abasi aliamuru ipigwe penalti ambayo ilipigwa kiufundi na mshambuliaji Mogarn Yeya na kufunga bao la pili na ushindi huku wakiwa na pointi nane mabao ya kufunga saba na nyavu zake zikiwa zimetinga mabao sita ikisaliwa na michezo miwili.
 
Ligi hiyo inaendelea tena April 18 mwaka huu kwa mchezo miwili baina ya JKT Mgambo Shooting na Transit Camp mchezo utaochezwa majira ya saa 8 mchana wakati ule wa saa 10 jioni utawakutanisha Tanzania Prinson dhidi ya Polisi Tabora.
 
Polisi Moro SC inaongoza kwa kuwa na pointi 14 ikifutiwa na JKT Mgambo Shooting pointi 12, Rhino Rangers, Mbeya City na Tanzania Prinson wote wakiwa na pointi nane kila mmoja wakitofautia mabao ya kufungwa na kufunga wote wakiwa na michezo sawa sita kila mmoja aliyokwisha cheza.

 
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: