MKUU WA MKOA WA MOROGORO, JOEL BENDERA KUSHOTO AKIPOKEA ZAWADI YA VITABU ZAIDI YA 2160 KUTOKA KWA MKURUGENZI MTENDAJI WA TAASISI YA NKWAMIRA SULTAINABLE LIFE TRUST YA DAR ES SALAAM, NORREN MAZALLA VYENYE THAMANI YA SH20MIL KATIKA HAFLA ILIYOFANYIKA OFISINI KWAKE MKOANI MOROGORO.
MKURUGENZI MTENDAJI WA TAASISI YA NKWAMIRA SULTAINABLE LIFE TRUST YA DAR ES SALAAM, NORREN MAZALLA AKIMKABIDHI MOJA YA VITABU KWA SHULE 10 ZA SEKONDARI AFISA ELIMU WILAYA YA MVOMERO I SALOME MWITUMBA KUSHOTO NA KATIKATI NI MKUU WA MKOA WA MOROGORO JOEL BENDERA.
MKUU WA MKOA WA MOROGORO JOEL BEBDERA AKIONYESHA SEHEMU YA VITABU MARA BAADA YA KUKABIDHIWA NA TAASISI HIYO, KULIA NI MKURUGENZI MTENDAJI WA TAASISI YA NKWAMIRA SULTAINABLE LIFE TRUST YA DAR ES SALAAM, NORREN MAZALLA
MKURUGENZI MTENDAJI WA TAASISI YA NKWAMIRA SULTAINABLE LIFE TRUST YA DAR ES SALAAM, NORREN MAZALLA KATIKATI AKIFAFANUA JAMBO KABLA YA KUTOA MSAADA HUO.
MAAFISA ELIMU WILAYA YA MVOMERO SALOME MWITUMBA KUSHOTO NA CLEA HAULE KUTOKA MOROGORO VIJIJINI KULIA KATIKA HAFLA HIYO AMBAYO SHULE 10 ZA SEKONDARI ZA AMBAZO ZIMENUFAIKA NA MSAADA HUO.
TAASISI ya kiraia ya Nkwamila Sultainable Life Trust ya jijini Dar es salaam inayojihusisha na ufadhiri wa elimu nchini umetoa msaada wa vitabu mbalimbali vyenye thamani ya 20 Mil kwa shule 10 za sekondari mkoani Morogoro ilikuweza kuinua kiwango cha elimu.
Akipokea msaada huo Mkuu wa Mkoa wa morogoro Joel Bendera alisema kuwa taasisi hiyo imetoa msaada huo wa zaidi ya vitabu 2160 nyenye zaidi ya thamani ya sh 20 Mil ambapo vitabu hivyo vitasaidia kuimarisha na kufanikiasha kazi ya ufudishaji kwa walimu wa shule hizo.
Alisema kupatikana kwa vitabu hivyo kutasaidia kuinua kiwango cha elimu katika shule hizo ambazo zilikuwa zikikabiliwa na upungufu mkubwa wa vitabu vya kiada na ziada ambapo ambapo kwa sasa kila mwanafunzi ataweza kutumia kitabu kimoja baada ya msaada huo.
Alizitaja shule za sekondari 10 zitakazonufaika na msaada huo katika wilaya za Mvomero na Morogoro Vijijini kuwa ni pamoja na Fatemi, Kinole, Mkulazi, Kiroka, Tegetero zote za Morogoro Vijijini na zingingine ni Mziha, Ng’ulu, Maskati, na Kikeo za wilayani Mvomero.
Bendera alisema kuwa shule nyingi sekondari zilizopo pembezoni mwa Mkoa wa Morogoro zimekuwa zikikabiliwa na upungufu wa vitabu vya kiada na ziada hivyo kusababisha kushusha kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi katika mitihani yao ya kuhitimu elimu ya kidato cha nne hari inayosababishwa na upungufu huo wa nyezo za kujifunzia.
“Naishukuru taasisi ya Nkwamira Sustainable Life Trust kwa kutoa msaada huu wa vitabu ambao ni zaidi ya 2,160 kwani utasaidia kuongeza chachu kwa wanafunzi kupenda kusoma nina imani kiwango cha ufaulu wa shule hizo 10 kitaongezeka” alisema Bendera.
Pia alisema kuwa licha ya msaada huo lakini bado shule za sekondari za Mkoani Morogoro zinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa nyumba za kuishi walimu, madawati kwa wanafunzi ambapo serikali inatarajia kushirikiana na wananchi kukabiliana na changamoto hizo.
Naye Mkurugenzi wa taasisi hiyo ya Nkwamila Sultainable Life Trust, Norren Mazalla alisema msaada huyo wa vitabu umegharimu kiasi cha sh 20Mil ambao umetolewa baada ya kufanyika kwa tafiti iliyofanywa na taasisi yake kwa kipindi cha miezi zaidi ya miwili na kubaini uhaba huo wa vitabu vya kiada na ziada.
Mazalla alisema vitabu vilivyotolewa kwa shule hizo vya aina tano tofauti kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne vikiwemo vya masomo ya Kiswahili, Kiingereza, Geografia,Uraia na masomo ya sayansi.
0 comments:
Post a Comment