Mlinzi wa timu ya soka ya darasa la tatu B shule ya msingi Bungo
Manispaa ya Morogoro, Mikidadi Mtanda (9) kushoto akijaribu kumiliki
mpira dhidi ya mshambuliaji wa timu ya darasa hilo A, Khalid Ramadhan
(9) kulia wakati wa michezo baada ya kumalizika kwa mitihani ya madarasa
kwa ajili ya kufunga shuleni ili wanafunzi kwenda likizo mkoani hapo.
MASHINDANO ya umoja wa michezo shule za msingi
Tanzania (UMITASHUMTA) ngazi ya mkoa wa Morogoro 2012 ambayo yanashirikisha wanamichezo
kutoka wilaya sita za mkoa huo yanaanza kutimua vumbi katika uwanja wa Jamhuri
mjini hapa kesho.
Kaimu Afisa Michezo mkoa wa Morogoro, Asteria Mwang’ombe
alisema kuwa mashindano hayo yanalengo kuibua na kuendeleza vipaji vya kila
aina ya michezo ikiwemo na kuchagua wachezaji kwa ajili ya kuunda vikosi
mbalimbali vya michezo ili kuweza kushiriki mashindano Umitashumta ngazi ya
kanda Kibaha mkoani Pwani.
Mwang’ombe alisema kuwa katika mashindano hayo
wilaya sita za mkoa huo tayari zimewasili katika Manispaa ya Morogoro kwa ajili
ya michuano hiyo ikiwemo wilaya ya Kilosa, Mvomero, Ulanga, Morogoro Vijijini,
Kilombero na mwenyeji Morogoro Manispaa ambapo washiriki watashindana katika michezo
ya soka, netiboli, mbio za riadha kuanzia mita 100 hadi mita 3000, mpira wa
wavu wavulana na wasichana, kurusha mitupo na kuruka pamoja na taaluma katika
darasa la tatu hadi darasa la sita.
“licha ya kuwepo kwa michezo hiyo pia tuna
wanamichezo wenye mahitaji maalumu katika michezo wa soka kati ya shule ya
msingi Kilakala kitengo cha viziwi na wenzao wa kitengo cha viziwi shule ya
msingi Kiwanja cha Ndege na maandalizi yote yamekamilika kwa ajili ya michezo
hiyo" alisema Mwang'ombe.
Mwang’ombe ametoa wito kwa wakazi wa Manispaa ya Morogoro kujitokeza kwa wingi katika uwanja wa Jamhuri katika mashindano hayo ili kuweza kuona vipaji vya watoto wao katika michezo hiyo hufanyika kila mwaka.
Mwang’ombe ametoa wito kwa wakazi wa Manispaa ya Morogoro kujitokeza kwa wingi katika uwanja wa Jamhuri katika mashindano hayo ili kuweza kuona vipaji vya watoto wao katika michezo hiyo hufanyika kila mwaka.
0 comments:
Post a Comment