Rais Dkt. Jakaya Kikwete, akiweka Ngao na
Mkuki kwenye Mnara wa Mashujaa, wakati wa maadhimisho ya siku ya
kumbukumbu ya Mashujaa, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja
jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera mkuki wakati wa
kilele cha maadhimisho ya siku ya mashujaa waliofariki dunia katika vita
ya Kagera
mwaka 1978 na 1979 yaliyofanyika kimkoa katika
mnara wa kumbukumbu wa Posta mjini hapa.
Mkuu wa
shule ya mafunzo ya huduma Pangawe Morogoro Kanali Harrison Masebo
akiweka shoka na sime katika mnara wa kumbukumbu wa mashujaa wakati wa
kilele cha maadhimisho ya siku ya mashujaa waliofariki dunia katika vita
ya Kagera
mwaka 1978 na 1979 yaliyofanyika kimkoa katika
mnara wa kumbukumbu wa Posta mjini hapa.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Saidi Thabiti Mwambungu akielekea katika mnara wa kumbukumbu kuweka ngao na mkuki wakati wa kilele cha kuwakumbuka mashujaa waliopoteza maisha katika vita vya maji maji mkoani humo.
Askari wa zamani wa jeshi la wananchi
Tanzania
(JWTZ) aliyewahikupigana vita kuu ya dunia, Edward Mahamba (99) akiongwa na
askari wa jeshi la wananchi kuelekea kuweka mkuki na upinde katika
mnara wa kumbumbuku wa mashujaa wakati wa kilele cha maadhimisho hayo.
Askari wa JWTZ mkoa wa Morogoro kikosi cha maombolezi wakitoa heshima zao katika mnara wa kumbukumbu wa Posta wakati wakiwakumbuka askari waliopoteza maisha katika vita ya
Kagera mwaka 1978 na 1979 mkoani hapa.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro Amir Nondo akiweka shada la maua katika mnara wa kumbukumbu wa mashujaa wakati wa
kilele kilele hicho.
Askari wa JWTZ akiwa katika maandalizi ya kutenga bomu la ardhini (picha ya pili kutoka chini) wakati mwisho ni Askari wa jeshi hilo wakiwa katika ukakamavuhuku mabomu yakiwa yanalipuka ikiwa ishara ya kuwakumbuka askari waliopoteza maisha katika vita katika kilele cha maadhimisho hayo.
0 comments:
Post a Comment