WAWINDAJI kutoka sehemu
mbalimbali barani Afrika hutumia mitego kwa ajili ya kunasa wanyama pori
kwa kitoweo, mitego hii ikiua au kumjeruhi mnyama yule.
Hata hivyo kuna baadhi ya masokwe wanaoishi
katika misitu ya Guinea ambayo wamejifunza jinsi ya kutambua mitego hhiyo na kwa mujibu wa wataalamu wanaofanya utafiti kuhusu nyenzo na tabia ya
sokwe.
La kustaajabisha ni kwamba sokwe pindu anaponasa katika mtego hujitahidi kutafuta na kuiharibu mitego bila madhara.
Ugunduzi wa tabia ya sokwe hao ulifanywa na
wataalamu wa masuala ya wanyama pori Gaku Ohashi na Tetsuro
Matsunzawa waliokuwa wakifuatilia tabia na nyenzo za sokwe huko Bossou
nchini Guinea.
Kuna ripoti nyingi za kujeruhiwa kwa sokwe wengi
Afrika mashariki na magharibi kukisababishwa na mitego ambapo wengi
wamekufa ndani ya mitego hiyo.
Hata hivyo kuna taarifa chache kuhusu
kujeruhiwa kwa sokwe wanaopatikana huko Bossou, jambo linaloshangaza kwa
sababu sokwe hawa wanaishi karibu na makaazi ya watu ambako mitego
hutumiwa mara kwa mara.
Wakati wataalamu wakifanya utafiti wao, Ohashi na Prof
Matsuzawa kutoka kitivo cha uchunguzi wa wanyama pori cha Chuo Kikuu cha
Kyoto Japan waligundua kuwa sokwe watano wa kiume wenye umri mdogo
na mmoja mkubwa walikuwa wanajaribu kuvunja na kuinasua mitego kadhaa.
Kwa mara mbili wataalamu hawa walishuhudia sokwe hawa wakifanikiwa kuinasua mitego iliyowekwa kuwanasa wao.
Nyaya
Mtego wa kawaida kwa mfano unaotengenezwa na kabila la Manon wa huko Bossou huundwa kwa waya wa chuma unayozungushwa kamba ya mimea ya msituni.
Nyaya hizi hazibagui ni mnyama gani anayenaswa.
Lakini sokwe wa kiume wa Bossou wamegundua jinsi ya kukwepa njama za wawindaji hao na
Kwa mujibu wa Ohashi alipozungumza na BBC
alisema kuwa sokwe hawa ni kama wanafahamu sehemu yenye hatari na sehemu
ambazo hazina tatizo na hivyo kufanikiwa kujiondolea hatari.
Mara nyingi sokwe hawa walishika kijiti cha
mtego na kukitikisa kwa nguvu hadi mtego ukaachia na mara nyingine
hugonga kijiti kinachoshikilia mtego na kusubiri kiachilie kisha huvunja
mtego mzima.
Hii ndiyo ripoti ya kwanza kuhusu sokwe wanaovunja na kuharibu mitego iliyokusudia kuwanasa na
Vile vile kitendo cha sokwe hawa kinaelezea kuwa sokwe wanaweza kujifunza na kufahamu.
Mara nyingi sokwe hujifunza kwa kujaribu bila
kujali athari yoyote. Mfano ni wanapojaribu kuvunja mbegu, hutumia jiwe
na wanapokosea hujaribu kutumia mikono bila kufanikiwa.
Majaribio ya aina hiyo hayangeweza kufanikishwa
juu ya mitego, sababu kosa moja lingesababisha kifo. Kwa hiyo ina maana
kuwa sokwe wanaweza kujifunza na kutumia mbinu ambayo haihatarishi
maisha yao, alisema Ohashi.
Wakati wote huu, sokwe wachanga walifuatilia
jinsi sokwe mkuu anavyofanya kabla ya kusogelea mtego ule na kuugusa
baada ya kuhakikisha kuwa ni salama kufanya hivyo.
Wataalamu hawa wanasema kuwa mitego hii ni
tishio kubwa kwa sokwe na wanaongoza juhudi za kuchambua misitu ili
kuondoa mitego yote iliyoko.
Wanasema pia kwamba sokwe kutoka maeneo mengine
hawajafikia kiwango cha wenzao wa Guinea katika kuondoa hatari
inayowakabili ya mitego ya wawindaji.
0 comments:
Post a Comment