BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

CCM KATA YA SABASABA MANISPAA YA MOROGORO YAPATA VIONGOZI WAPYA.

Diwani wa chama cha mapinduzi (CCM) kata ya Mbuyuni Manispaa ya Morogoro, Samuel Msuya kushoto akimsikiliza Mwenyekiti mpya wa chama chicho kata ya Sabasaba, Mudhili Shoo (katikati) akizungumza jambo mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa kuchagua viongozi mbalimbali ndani ya kata hiyo iliyofanyika katika mtaa wa Ngoto mkoani hapa kulia ni Diwani wa kata ya Kilakala kupitia chama hicho Libon Mkali.
Hapa Mwenyekiti huyo, Mudhili Shoo kulia akiteta jambo na Mhe Diwani Msuya kushoto baada ya kumalizika kwa uachaguzi huo.
Mhe Msuya akitangaza matokeo ya uchaguzi huo katika nyasfa mbalimbali.
 Sehemu ya wajumbe wa uchaguzi huo wakifuatilia matukio mbalimbali ndani ya ofisi za kata hiyo ya Ngoto mkoani hapa.


CHAMA cha mapinduzi kata ya Sabasaba Manispaa ya Morogoro imepata viongozi wapya wataongoza kata hiyo kwa miaka mitano baada ya kufanyika kwa uchaguzi wa kuchagua viongozi wa ngazi mbalimbali ndani ya kata hiyo mkoani hapa.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo Msimamizi mkuu wa uchaguzi huo, Samuel Msuya alimtangaza, Mudhili Shoo, kuwa mwenyekiti mpya wa chama hicho katika kata hiyo baada ya kupata kura 38 akimshinda mpinzani wake katika nafasi hiyo John Mirambo aliyepata kura saba.

Msuya aliwatangaza wajumbe watatu wa halmashauri kuu ya kata kuwa ni Haruni Kikoro aliyepata kura 41, Mrisho Swed, akipata kura 41 na Salehe Komba kura 38.

Katika nafasi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa ccm wilaya ni pamoja na, Dotto Kiswili kura 39, Salehe Komba kura 37, Agness Mluge kura 36, Jamila Mihengo kura 36, Abdallah Malongoza kura 34, Abubakari Chunda kura 33, Ally Marjeby kura 33, Anthonia Miti kura 31, Ramadhan Chamcha kura 31, na Mengi Mbilikila kura 29.

Aidha mara baada ya kukamilika kwa uchaguzi huo Mwenyekiti huyu aliyeingia madarakani aliendesha uchaguzi wa kuchagua viongozi wengine katika nafasi tatu tofauti ikiwemo ya katibu mwenezi na siasa ambayo, Charles Tunge aliibuka kwa kuchaguliwa tena kwa kupata kura 33 akimshinda mpinzani wake Abdallah Lukanda aliyepata kura moja.

Wakati Bashiri Kikoro akichaguliwa kushika nafasi ya katibu mwenezi na siasa kata kufuatia kupata kura 34 dhidi ya Jumanne Mhando akipata kura nne.

Shoo alimtangaza,Nuru Majitaka kuwa katibu uchumi na fedha baada ya kupata kura 18 kutoka kwa wajumbe wa mkutano huo akiwashinda wenzake, Dotto Kiswili aliyepata kura 11 na Yusuph Mgoh aliyeambulia kwa kupata kura tano.

Mwenyekiti huyo alisema kuwa viongozi waliochaguliwa katika ngazi mbalimbali ndani ya kata hiyo kutumikia nyasfa hizo na kuwa mfano mzuri wa kuigwa kwa mwananchi ndani na nje ya kata hiyo kwa kusimamia sera zinazoongoza chama hicho na kuanza kwa kutoa ushirikiano mzuri kwa kuhamamisha  wananchi kuhesabiwa wakati wa zoezi la sensa ya watu na makazi kuwa jambo hilo ni muhimu katika mipango ya maendeleo kwa Agosti 26 mwaka huu.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: