WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA akiwahutubia wananchi waliojitokeza katika ufunguzi wa maonyesho ya wakulima kanda ya mashariki inayoundwa na mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani na Morogoro katika viwanja vya Mwl Julius Nyerere Nane Nane mkoani Morogoro.
Waziri mkuu Mizengo Pinda kulia akipata maelezo kutoka kwa
Mkurugenzi Mtendaji
wa Tanseed International, Isaka Mashauri juu ya mbegu ya zao la mpunga
aina ya TXD 306 (SARO5) wenye uwezo wa mavuno tani sita kwa hektari moja
wakati waziri mkuu huyu
alipotembelea banda kampuni ya uzalishaji wambegu bora za mahindi katika
maonyesho ya wakulima ya nane nane kanda ya mashariki uwanja wa Mwl
Julius Nyerere mkoani Morogoro.
Pinda
kulia akiangalia kilimo mseto cha mahindi na mbaazi wakati alipotembelea
banda hilo la Tanseed Internationali kushoto
ni Mkurugenzi Mtendaji
wa kampuni hiyo, Isaka Mashauri na
katikati ni Mwenyekiti wa Taso kanda ya Mashariki, Mohamed Mzee.
Hapa Pinda akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji
wa kampuni ya mbegu bora ya Tanseed International Morogoro, Isaka Mashauri juu ya teknolojia ya mbegu ya
mahindi ya chakula malisho (FOOD-FEED) katika banda hilo wa kwanza kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel
Bendera.
Waziri mkuu Mizengo Pinda na Mwenyekiti wa Taso kanda ya Mashariki, Mohamed Mzee kulia wakati msafara wa mkuu huyu ulipofika katika banda Water for Third word (W3W)katika maonyesho hayo.
Waziri mkuu Mizengo Pinda kulia, Katibu wa Taso Raphael Jackson na mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera wakati kutembelea mabanda ya maonyesho mbalimbali katika ufunguzi huo.
1 comments:
safi sana hyo
Post a Comment