BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WAZIRI MKUU MELES ZENAWI WA NCHI YA ETHIOPIA AFARIKI DUNIA

Waziri mkuu Meles Zenawi amefariki dunia jumatatu usiku akiwa na umri wa miaka 57 kutokana na ugonjwa usojulikana wakati akipata matibabu katika nchi ya kigeni.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi habari mjini Addis Abeba Jumanne, msemaji wa serikali Bereket Simon hakutoa maelezo zaidi juu ya ugonjwa wa Meles ama wapi alikuwa akitibiwa.

Hata hivyo ameleza kwamba waziri mkuu alikua anauguwa tangu mwaka jana na kwamba mkewe na watoto wake walikuwa pamoja nae alipofariki.

"Baada ya wiki kumi za matibabu katika nchi ya kigeni alifariki jana kiasi cha usiku wa manane na mwili wake utarudishwa nchini Ethopia hivi karibuni kwa mazishi," alisema. Bereket

Bereket aliwambia waandishi wa habari kuwa naibu waziri mkuu na waziri wa mambo ya nchi za nje, Hailemariam Desalegn ataapishwa kuwa waziri mkuu mpya wa Ethopia na kuwa hapatakuwepo na uchaguzi kwani katiba inamruhusu naibu waziri mkuu kuchukua madaraka moja kwa moja.

Meles Zenawi hakuonekana hadharani tangu mwishoni mwa mwezi wa June na Serikali ya Ethopia ilisuta uvumi kwamba alikuwa katika hali mahtuti.
 
Alipokuwa akisomea udaktari, Meles (anayeitwa kwa jina lake la kwanza kama ilivyo ada nchini Ethiopia), alianza kujihusisha na mausala ya kisiasa.

Alijiunga na makundi yanayofuata mafundisho ya mwanafalsafa Karl Marx. 
Aliungana pia na vuguvugu lililosababisha kung'olewa madarakani kwa mfalme Haile Selassie mwaka 1974.
Muasi awa Waziri Mkuu

                             Zenawi (kushoto) na Rais Mwai Kibaki wa Kenya.  
                  Zenawi (kushoto) na Rais Mwai Kibaki wa Kenya.
 
Baada ya Mengistu Haile Mariam kuingia madarakani, Meles alikatisha masomo yake na badala yake kuingia katika vita vya chini kwa chini dhidi ya Mengistu. 

Kwa zaidi ya miaka 10, kundi lake la waasi liitwalo Tigray's People Liberation Front (TPLF), lilifanya mashambulizi katika milima ya Tigray na mwezi Mei 1991 waasi wa kundi la TPLF wakisaidiwa na Marekani walifanikiwa kuuteka mji mkuu Addis Ababa.

 Meles aliyekuwa rais wa kipindi cha mpito alipoulizwa na gazeti la nchini Ujerumani la Frankfurter Rundschau kama nchi yake iko tayari kwa demokrasia alijibu.

"Hivi mnafahamu kwamba nchi yetu ilikuwa na utamaduni ulioendelea kabisa wakati ninyi mlikuwa bado wawindaji na watu wakukusanya matunda na mboga msituni?" alihoji Meles.

Meles alichaguliwa kuwa Waziri Mkuu wa Ethiopia na muungano wa vyama uliokuwa madarakani tangu mwaka 1991nchini Ethiopian Peoples' Revolutionary Democratic Front (EPRDF) na  ulianza kuwasaka washirika wa Mengistu. 

Tangu kuingia madarakani kwa Meles,mashirika ya kutetea haki za binadamu yamekuwa yakilaani sera zake hasa juu ya namna alivyoiendesha nchi yake katika miaka ya 1990 lilipotokea janga la njaa.
 
Mfano bora wa mwanzo mpya barani Afrika?

Matukio mawili makuu yalimaliza kabisa dhana kwamba Meles ndiye tumaini la mwanzo mpya Afrika.
Tukio la kwanza ni vita kati ya Ethiopia na nchi jirani ya Eritrea vilivyotokea kati ya mwaka 1998 na 2000.

Tukio la pili ni wizi wa kura katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka 2005 na watu wapatao 200 waliuwawa kwenye maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi huo. 

Wakati Meles alipokuwa akijisifu kwa kuwapataia raia wake haki ya kufanya uchaguzi aliouita wa haki maafisa wake wa usalama waliwashambulia kwa risasi wanafunzi waliokuwa wakiandamana na kuwaua.

Baada ya uchaguzi wa mwaka 2005 mashirika ya kutetea haki za binadamu yaliripoti juu ya rushwa na matumizi ya nguvu dhidi ya wapinzani. 
Tarehe 12 Juni mwaka 2012 waandishi wa habari wapinzani na wanaharakati 24 walihukumiwa chini ya sheria mpya ya kupambana na ugaidi. 

Mwandishi mmoja wa blogu alihukumiwa kifungo cha miaka 18 na utawala wa Meles unashutumiwa pia kwa kutumia fedha za misaada kwa ajili ya kampeni ya uchaguzi.

Kiongozi mwenye sura mbili
Meles, ambaye alikuwa anapendelea kusoma, kuogelea au kucheza tenisi katika muda wake wa mapumziko, alikuwa na kipaji cha kuzungumza mbele za watu. 

Kipaji hicho kinaonyesha pande mbili za kiongozi huyu nchini mwake alikuwa kingozi asiyesita kuzima upinzani wowote dhidi yake, ikibidi hata kwa kutumia nguvu. 

Lakini katika majukwaa ya kimataifa alijionyesha kuwa msemaji wa bara la Afrika, akizungumzia masuala kama vile mabadiliko ya tabia nchi na athari zake kwa bara la Afrika.

Hata hivyo yapo mambo ya maendeleo aliyowaletea wananchi wake, maendeleo katika sekta ya elimu na sekta ya afya yakiwa miongoni mwa hayo. 

Kiujumla, Ethiopia ilijipatia maendeleo mengi chini ya utawala wake, licha ya kwamba maendeleo mengi yalikwamishwa na ongezeko la kasi la idadi ya watu nchini humo na uchumi wa Ethiopia unakua kwa haraka, lakini wanaofaidika zaidi ni viongozi wa kisiasa.

Afya ya Meles
Kwa muda mwingi kumekuwepo na tetesi juu ya kuugua kwa Meles na Mara kwa mara kiongozi huyo alilazimika kwenda nje ya nchi kwa matibabu.

 Aliposhindwa kuhudhuria mkutano mkuu wa Umoja wa Afrika uliofanyika Julai 2012 mjini Addis Ababa, ulizuka uvumi juu ya kifo chake na kulazimika msemaji wake kukanusha taarifa hizo.

Meles Zenawi alifariki dunia Jumanne, 21.08.2012. Amemwacha mke wake Azeb Mesfin na watoto watatu.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: