Kwa ufupi.
“Tumekuwa tukipokea simu nyingi kutoka kwa watu
mbalimbali wakihitaji kufahamu ukweli kuhusu tukio la kupigwa risasi kwa
mtumishi wa Takukuru, Bhoke Ryoba,” imesema sehemu ya taarifa hiyo ya
Dk Hoseah iliyotolewa na ofisi ya habari ya Takukuru.
OFISA uchunguzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Bhoke Ryoba, ameuwawa kwa kupigwa rasisi na watu wasiojulikana.
Mkurugenzi wa Takukuru Dk Edward Hoseah
OFISA uchunguzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Bhoke Ryoba, ameuwawa kwa kupigwa rasisi na watu wasiojulikana.
Habari zilizolifikia gazeti hili jana zilieleza
kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana eneo la Kigamboni
Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam, ambako ofisa huyo alikuwa
anahudhuria sharehe.
Mkurugenzi wa Takukuru Dk Edward Hoseah, akizungumzia tukio hilo alithibitisha na kueleza kuwa alifariki dunia juzi usiku.
“Tumekuwa tukipokea simu nyingi kutoka kwa watu
mbalimbali wakihitaji kufahamu ukweli kuhusu tukio la kupigwa risasi kwa
mtumishi wa Takukuru, Bhoke Ryoba,” imesema sehemu ya taarifa hiyo ya
Dk Hoseah iliyotolewa na ofisi ya habari ya Takukuru.
Iliendelea, “Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru Dk Edward
Hoseah, anapenda kutoa ufafanuzi kuhusu tukio hili kwamba ni kweli
mtumishi Bhoke Ryoba amefariki dunia jana usiku, Jumamosi Desemba 22,
2012 baada ya kupigwa risasi. Uchunguzi wa Polisi kuhusu chanzo cha
tukio hilo bado unaendelea”.
Baadaye ofisa habari wa Takukuru Doreen Kapwani
alifafanua kuwa ofisa huyo mchunguzi alifikwa na umauti wakati
anajumuika na marafiki zake katika moja ya tafrija iliyokuwa ikifanyika
katika eneo la Kigamboni.
Alisema akiwa katika hafla hiyo, ghalfa walitokea watu wasiojulikana na kumiminia risasi hadi kufa.
“Hawa watu walimvamia Ryoba aliyekuwa kwenye
sherehe moja na kumshambulia kwa risasi na kisha wakatokomea
kusikojulikana,” alisema na kuongeza.
“Watu hao hawakutambulika kwa kuwa baada ya kutekeleza azma hiyo walitoweka haraka na kutokomea.”
Alipotakiwa kueleza pengine kumekuwepo matukio
yoyote katika siku za hivi karibuni yanayoweza kusababisha tukio hilo,
Kapwani alijibu “ni mapema mno sasa kudadisi suala hilo.”
Kapwani alisema Ofisi ya Takukuru kwa sasa haiwezi kueleza chochote kwani tukio hilo limeripotiwa polisi kwa uchunguzi zaidi.
Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam,
Suleman Kova alipotakiwa kuelezea hatua zilizochukuliwa na jeshi hilo
baada ya tukio hilo, alisema kuwa hangeweza kuzungumzia chochote kwa
vile alikuwa nje ya ofisi.
0 comments:
Post a Comment