Mtu aliyejitambulisha kuwa askari wa Jeshi la wananchi wa Tanzania
(JWTZ),kambi ya Monduli,Arusha akiwa na wabunge wa Chadema,Godbless Lema
(Arusha Mjini) na Joshua Nassari (Arumeru Mashariki) baada ya
kumalizika kwa mkutano wa hadhara uliohutubiwa na wabunge hao katika Mji
mdogo Mererani,Simanjiro mkoani Manyara jana.
MBUNGE wa Arusha Mjini (Chadema) Godbless Lema, huenda akazo
kitita cha Sh85 milioni ambazo ni malimbikizo ya mishahara na posho
mbalimbali ambazo hakulipwa wakati alipokuwa nje ya Bunge.
Lema amekuwa nje ya Bunge kwa miezi minane,
kuanzia Aprili 5 mwaka huu wakati alipovuliwa ubunge na Mahakama Kuu
Kanda ya Arusha, hadi aliporejeshewa ubunge wake Ijumaa wiki iliyopita
na Mahakama ya Rufani ambayo ilikubali rufaa yake iliyopinga uamuzi huo.
Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah jana
alisema baada ya kurejea bungeni, Lema atalipwa stahili zake zote
anazostahili kwa muda wote wa siku 260 ambao alikwa nje ya Bunge.
Ingawa ofisi hiyo ya bunge haikusema atalipwa
shilingi ngapi, uchambuzi wa malipo na stahili za wabunge umebaini kuwa
mbunge huyo kupitia Chadema, atalipwa kitita cha Sh85 milioni ikiwa ni
mshahara wake na posho kwa kipindi cha miezi nane alichokuwa nje ya
Bunge.
Hata hivyo, Lema mwenyewe aliliambia gazeti hili jana kuwa, malipo yake yanaweza kufikia Sh60 milioni.
Lema aliyeibuka mshindi katika Uchaguzi Mkuu wa
mwaka 2010, alivuliwa wadhifa huo na Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha,
April 5, 2012, kufuatia kesi iliyofunguliwa na makanda watatu wa CCM.
Mussa Mkanga, Happy Kivuyo na Agness Mollel, wakipinga ushindi wake.
Hata hivyo, Desemba 21,2012, Mahakama ya Rufani ilimrejesha bungeni, baada ya kushinda rufaa yake aliyokata mahakamani hapo kupinga hukumu na tuzo ya Mahakama Kuu Arusha iliyomvua wadhifa huo.

Tangu alipovuliwa ubunge hadi Mahakama ya Rufani
ilipomrejesha tena bungeni, Lema alikuwa amekosa mikutano mitatu ya
Bunge yenye jumla ya vikao 84.
Mikutano hiyo ni ule wa mwezi Aprili, mkutano wa Bunge la Bajeti Juni hadi Agosti na mkutano wa Novemba.
Mikutano hiyo ni ule wa mwezi Aprili, mkutano wa Bunge la Bajeti Juni hadi Agosti na mkutano wa Novemba.
Vyanzo vya kuaminika kutoka ndani ya Bunge na
wakiwamo wabunge wa upinzani na wale wa CCM vilisema kwamba malipo ya
mbunge kwa mwezi ni Sh10.7 milioni, yakijumuisha Sh2.3 milioni za
mshahara, Sh2.5 milioni za mafuta, posho ya jimbo inayokaribia Sh5
milioni na malipo mengineyo.
Kwa muda wa miezi zaidi ya minane ambao amekuwa
nje ya Bunge, malimbikizo ya mshahara wake yanafikia Sh18.4 milioni,
posho ya jimbo Sh40 milioni, mafuta Sh20 milioni na posho nyingine Sh6.6
milioni.
Kauli ya Lema
Hata hivyo akizungumza na Mwananchi jana, Lema alisema kuwa ingawa hajui kwa hakika kuwa malipo yake ni kiasi gani, lakini kwa hesabu za haraka, yanafikia Sh60 milioni.
Alisema wakati wa kesi hiyo ikiendelea hakuwahi kuwaza kwamba angerejeshwa bungeni, hivyo hakuwahi atalipwa kiasi gani na Bunge.

“Sijui kwanza nitalipwa nini kwani sikuwahi kukaa
na kupiga hesabu za malipo haya, maana najua ubunge siyo faraja bali
ni kuongoza harakati za kuwasaidia wananchi kutetea haki zao
mbalimbali,” alisema Lema.
Alisema alichokuwa akijua ni kwamba kama
akishinda basi, atarejeshewa gharama za kesi yake na makada wa CCM ambao
walimfungulia kesi kwani ni malipo yanayotambulika kisheria.
“Najua lazima hawa makada wa CCM, walipe gharama zangu za kesi.Baada ya wao kushinda kesi Mahakama Kuu, Arusha, waliniletea madai ya kuwalipa Sh139 milioni na sasa mimi nawadai zaidi ya milioni 250,” alisema Lema na kuongeza.

0 comments:
Post a Comment