BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KOCHA WA BANDARI ALAZWA.

KOCHA WA BANDARI FC, RISHADI SHEDU.


ABDULRAHMAN SHERIFF.
 
KOCHA wa Bandari FC, Rishadi Shedu, aliyeirudisha timu yake Ligi Kuu Kenya, leo Jumamosi atalazwa katika Kituo cha Kikuyu Orthopedic Rehabilitation Centre kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa kuunganishwa mifupa kati ya kisigino na goti.

Akizungumza kwa njia ya simu akiwa jijini Nairobi, Shedu alisema kwamba anatarajia kubakia hospitalini hapo kwa siku nne ama tano kabla ya kuruhusiwa kwenda nyumbani.

Baada ya hapo atatakiwa pia kupumzika kwa wiki sita kabla ya kuanza kazi ya kuiandaa timu yake kwa ajili ya majukumu makubwa ya msimu ujao.

"Ni suala la kufuata maelekezo ya madaktari tu.

Lakini wakati wote wa kujiuguza nitakuwa nawasiliana na maofisa wengine wa timu kuhusu mipango ya mazoezi na mambo mengine ya wachezaji," alisema.

Kwa sasa timu hiyo iko mapumzikoni hadi Desemba Tatu itakapoanza mazoezi katika Uwanja wa Mbaraki.

Bandari imerejea ligi kuu baada ya kutwaa ubingwa wa Kanda A ya Ligi Daraja la Kwanza iliyomalizika hivi karibuni.

Wakati huohuo, Shedu amemtumia salamu za kumtakia heri mshambuliaji wake, Erick Okoth, aliyelazwa katika hospitali ya Aga Khan ya mjini Mombasa anakotibiwa maradhi ya kifua.

Naye nahodha wa timu hiyo, Raphael Okello, anaendelea kupata matibabu katika kituo cha AAR baada ya kuumia goti kwenye mechi dhidi ya Sparki Youth. Pia Watanzania, Meshack Abel na Mohamed Banka wanaugulia misuli ya paja.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: