BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KUELEKEA KRISMAX WAFANYABIASHARA WAPANDISHA BEI YA VYAKULA.


KWA UFUPI

Maandalizi ya sikukuu bei juu

Bei ya maharage zimepanda kutoka Sh1,600 kwa kilo hadi kufikia Sh2,100, mchele umepanda kutoka Sh1,800 kwa kilo hadi kufikia Sh2,400, unga wa ngano umepanda kutoka Sh1,200 kwa kilo hadi kufikia Sh 1,500 kwa kilo.
MAANDALIZI ya sikukuu za mwisho wa mwaka zimeingia dosari baada ya bei ya bidhaa za chakula kupanda kwa kiwango cha juu nchini.Mwanachi limefanikiwa kufanya uchunguzi na kugundua bei za vyakula zimepanda kwa kiasi kikubwa wakati huu wa kuelekeakatika sikukuu na kusababisha usumbufu kwa baadhi ya wananchi.

Bei ya bidhaa kama unga wa sembe umepanda kutoka Sh1,000 kwa kilo hadi kufikia Sh1,400 kwa kilo tofauti na awali huku wafanyabiashara hao wakijitetea kupanda kwa bidhaa hizokunatokana na msimu wa sikukuu.

Bei ya maharage zimepanda kutoka Sh1,600 kwa kilo hadi kufikia Sh2,100, mchele umepanda kutoka Sh1,800 kwa kilo hadi kufikia Sh2,400, unga wa ngano umepanda kutoka Sh1,200 kwa kilo hadi kufikia Sh 1,500 kwa kilo.

Wakizungumza na Mwananchi kwa nyakati tofauti wafanyabiashara wa soko la nafaka jijini Dar es Salaam, walisema kuwa hali hiyo inachangiwa na tabia ya kuwepo kwa baadhi ya wafanyabiashara kuwa na tabia ya kupandisha bei ya vitu hasa pale inapofikia msimu wa sikukuu.

Joshua John ,mfanyabiashara katika soko la Tandale, alisema kuwa kuna baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa na tabia ya kupandisha bei kila inapofika msimu wa sikukuu kwa sababu zao binafsi hata kama nafaka hazijapanda kwa sababu wameshazoea kuwa ndicho kipindi kizuri cha kuvuna pesa kutoka kwa wateja.

Nao wateja waliokuwepo sokoni hapo, Jackline Shoo alidai kusikitishwa na tabia ya wafanyabiashara hao kuwa na tabia ya kupandisha bei kiholela hususani wakati wa sikukuu hali inayowafanya wabadili ratiba za matumizi ya pesa ili waweze kujikimu kimaisha na familia zao.

“Sijui kwa nini hawa wafanyabiashara wanakuwa na tabia ya kupandisha bei za bidhaa hususani wakati wa sikukuu hali inayotulazimu tubadili matumizi ya pesa ili tuweze kujikimu na familia zetu” alisema Shoo

Hata hivyo baadhi ya wateja wanaopata huduma sokoni hapo wameitaka mamlaka husika ambayo ni wizara ya biashara na viwanda kusimamia na kufuatilia tatizo hilo kwa umakini kwani kitendo hicho kinawakosesha amani kila inapofika misimu ya sikukuu.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: