BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MAREKANI YAIHIMIZA KENYA KUTAFUTA SULUHU YA MAPIGANO YA KIKABILA.

 Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Kipao mkoa wa Tana River nchini Kenye wakiangalia miili ya wanaume waliouwawa wakati wa mapigano ya kikabila hivi karibuni.Wakazi wa Tana River katika eneo lililokumbwa na mapigano ya kikabila.Baadhi ya wakazi wa kijiji hicho wakihama kukimbia mapigano hayo.Wafanyakazi wa Msalaba Mwekundu wakiwa wamebeba mmoja wa watu katika tukio hilo kwa ajili ya huduma.

 Watoto wa kijiji cha Kipao wakiwa hospitalini baada ya kujeruhiwa katika vurugu hizo za mapigano ya kikabila katika mkoa wa Tana River nchini Kenya. 

SERIKALI ya Marekani imeeleza kusikitishwa kwake na mapigano mapya ya kikabila yaliyozuka juzi ijumaa katika kijiji cha Kipao mkoa wa Tana river pwani ya Kenya, kati ya makabila ya Orma na Pokomo na kusababisha vifo vya watu takribani arobaini na tano mpaka hivi sasa.

Msemaji wa Ikulu ya Marekani Jay Carney amesema Marekani imesikitishwa sana na mauaji hayo na inatoa wito kwa serikali ya Kenya, polisi na viongozi wa makabila hayo kuhakikisha wanapata suluhu ya mgogoro wa eneo hilo ambao pia ulisababisha mauaji ya watu zaidi ya mia moja katika mapigano yaliyozuka mwezi agosti mpaka septemba mwaka huu.

Taarifa iliyothibitishwa na polisi imesema vifo vimeongezeka toka thelathini na tisa juzi na kufikia arobaini na tano.

Mkoa wa Tana River umekuwa ukikumbwa na mapigano ya kikabila kati ya makabila hasimu ya wafugaji wa Orma na wakulima wa Pokomo na baadhi ya watu wamekuwa wakihusisha mapigano hayo na maswala ya kisiasa hususani katika wakati huu ambapo Taifa hilo lipo katika maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwezi machi mwaka ujao
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: