MIKE TYSON kulia akiwajibika ulingoni dhidi ya mpinzani wake.
MIKE TYSON.
BROOKLYN, MAREKANI.
BINGWA wa zamani wa masumbwi wa uzito wa juu, Mike 'Iron' Tyson anadaiwa kubadilisha jinsia na kuwa mwanamke, ambapo upasuaji wake umefanyika salama mwishoni mwa wiki iliyopita.
BINGWA wa zamani wa masumbwi wa uzito wa juu, Mike 'Iron' Tyson anadaiwa kubadilisha jinsia na kuwa mwanamke, ambapo upasuaji wake umefanyika salama mwishoni mwa wiki iliyopita.
Kwa
mujibu wa mtandao wa Newsbiscuits wa Marekani, upasuaji wa mabadiliko
ya jinsia ya mwanamasumbwi huyo wa zamani umefanyika katika kliniki ya
karibu na Beverley Hills.
Wakati alipokuwa katika mchezo huo, Tyson
alikuwa akijulikana kama ‘The Baddest Man on the Planet’ (Mtu mbaya
kuliko wote duniani), akiwa mzaliwa wa jiji la Brooklyn.
Na
bondia huyo inadaiwa aliwaambia waandishi kuwa kupata hedhi kwa mara
yake ya kwanza ni kama ndoto iliyokuwa kweli katika maisha yake, na
kuanza siku aliyofanyiwa upasuaji huo atakuwa akijulikana kwa jina la
Michelle.
Tyson
alinukuliwa akisema: "Baadhi ya watu walidhani kuwa ni hatari kwa mimi
kuwa mwanamke.
Tyson ambaye amefanyiwa upasuaji wa kubadilisha vitu
kadhaa vya kiume katika mwili wake saa 28 zilizopita anajisikia vizuri
kuwa hivyo.
"Lakini
hata muda mrefu nilioutumia katika mchezo wa masumbwi nilikuwa
nikijivunia kuwa bondia bora duniani siku zote, sikuwa na wazo
lililoingilia nilichokuwa nikifanya kwa wakati huo, lakini nilijua siku
moja nami natakuwa na matiti na uke."
Iron
Mike au Iron Maiden kama ambavyo anataka kuitwa sasa aliruhusiwa
kufanyiwa upasuaji na madaktari baada ya kuchunguzwa juu ya mwili wake,
ambapo katika historia yake, bondia huyo alilalamikiwa kwa kupigwa na
Evander Holyfield 1996.
Licha
ya Tyson kusema yuko vizuri kuendelea na pambano, mwamuzi Mitch Halpern
alilazimika kulimaliza katika raundi ya 11 akidai kuwa alimuona Tyson
kama aliyeshindwa kuendelea kwa usalama wake.
Tyson,
alionekana akiwa amevalia nywele za bandia za kike (wigi) na suruali
aina ya jeans ya bluu na fulana ya mwanamitindo Vanessa Bruno.
Alinukuliwa
akisema kuwa hali hiyo ya muonekano wake utasaidia kuwashawishi
Wamarekani kujua kuwa siku zake za umwamba ulingoni zimekwisha na
amekuwa mtu mwingine.
"Nimeuhifadhi
uume wangu katika chombo maalum kisichoozesha chumbani kwangu kwa ajili
ya kukumbuka viungo hivyo vilivyotufanya wakati tuko vijana wadogo
gerezani" alisema Tyson katika kauli tata.
Licha
ya watangazaji wengi wa ngumi kushindwa kutangaza alivyokuwa akivaa
akiingia katika mapambano yake, ilikuwa ni dalili tosha ya kuonesha kuwa
alitamani siku moja kuwa mwanamke.
Alama
hizo ni kama kuvaa viatu virefu vyenye nakshi za kike, aina fulani za
hereni na nguo ya juu kama gauni refu lenye urembo mwingi na hata katika
glovu zake kulikuwa na kama rangi za kucha.
0 comments:
Post a Comment