MWANARIADHA mlemavu wa Afrika Kusini na nyota wa
Olimpiki,Oscar Pistorius, amefikishwa mahakamani akikabiliwa kwa madai
ya kumuua mchumba wake baada ya kupigwa risasi akiwa nyumbani kwa
Pistorius mjini Pretoria.
baada ya kufikishwa maghakamani , wakala wa Oscar alikanusha madai hayo vikali.
Nyumba ya mwanariadha huyo iliyo katika eneo la kifahari mjini Pretoria.
mwaka jana Pistorius alikuwa mwanaruiadha wa kwanza mlemavu kuruhusiwa kushindana na wanariadha wengine wasio na ulemavu kwenye micheco ya Olimpiki, kwam kutumia miguu bandia.
amekuwa na uhusiano na mchumba wake marehemu, Reeva Steenkamp tangu Novemba mwaka jana,na walijulikana na wapenzi wenye kusifika sana nchini humo.
Wataalamu wa uchunguzi, wanatarajiwa kuendelea na uchunguzi wao katika nyumba ya Pistorius ambako mchumba wake Steenkamp, aliuawa.
Duru zinasema kukamatwa kwa Pistorous kumewashangaza wengi sana Afrika Kusini ambako anatazamiwa kama shujaa.
Awali duru zilisema kuwa Pistorius huenda alimuua Reeva Steenkamp kimakosa kwa kudhania kuwa ni mwizi aliyekuwa amemvamia, ingawa polisi walipuuza madai hayo.
Polisi walisema kuwa kumekuwa na visa kadhaa vilivyoriptiwa kutokea nyumbani kwa Pistorius na kutajwa kuwa ugomvi wa kinyumbani.
Pistorius anasifika kama mwanaridha wa kwanza mlemavu kushiriki michezo ya Olimpiki.
Habari za mauaji ya mpenzi wake Pistorius zimewashangaza wengi Afrika Kusini kwani anasifika kama mwanaridha anayeiletea nchi hiyo sifa.
Afrika Kusini ni moja ya nchi zenye visa vingi vya uhalifu duniani na watu wengi wanamiliki silaha za kujilinda.
0 comments:
Post a Comment