BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

TASWIRA YA VURUGU ZA BODABODA KUFUNGA BARABARA MASIKA KWA KUWEKA VIZUWIZI MOROGORO.

Askari wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Morogoro akiondoa gogo lililowekwa barabarani eneo la Masika baada ya waendesha pikipiki maarufu kama (Bodaboda) kufunga barabara kwa kuweka vizuwizi na kuchoma moto magurudumu wakipinga vitendo vya wafanyakazi wa mamlaka ya mapato (TRA) kudaiwa kuwavamia waendesha pikipiki hao huku pikipiki zikiwa katika mwendo na kusababisha ajali wakati wakikakagua mapato mkoani hapa.
 Raia wema wakiondoa jiwe lililokuwa limwekwa barabara kama kizuwizi wakati wa vurugu zilizdumu kwa muda wa dakika 45.
Askari kanzu aliyefahamika kwa jina la Rajabu Selemani akiondoa jiwe katika barabara lililowekwa na waendesha pikipiki hao.
Magurudumu yakiwa yamewekwa katikati ya barabara eneo hilo katika baraara itokayo Msamvu kuingia katika mzunguko wa Masika.
 Askari wa kikosi cha zimamoto wakizima moto wa uliowashwa na waendesha pikipiki (Bodaboda)
 Askari ya usalama wa barabarani akiondoa gurudumu kutoka barabarani na kuweka kando ya barabara ili magari yaweze kupita
 Askari kanzu na wenye sare wakidhibiti hali ya ulasama eneo hilo.
 Mkuu wa kituo cha Polisi kata Manispaa ya Morogoro, Iddi Ibrahim akiwa eneo la tukio.
Gari la Zimamoto likiwasili eneo la tukio ili kuweza kuzima moto huo, tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 6 mchana ambapo jeshi la polisi walifanikiwa kuwadhibiti waendesha pikipiki hao na kuendelea kwa magari kupita.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: