Mgombea kiti cha Urais nchini Kenye, Uhuru Kenyatta.
MMOJA wa wagombea kiti cha rais katika uchaguzi mkuu ujao nchini Kenya –Uhuru Kenyatta anasema yuko tayari kukubali matokeo iwapo wakenya wataamua kumchagua mgombea mwingike kuongoza taifa hilo.
Bwana Kenyatta anayekabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Waziri Mkuu Raila Odinga katika uchaguzi huo amekosoa wapinzani wake waliodai huenda kuna njama ya udanganyifu wa kura.
Hii ni kufutia madai yaliyoibuka kutoka upande mmoja wa kisiasa kulalamika kwamba mipango inafanywa ikisaidiwa na maafisa kadhaa kushinda katika uchaguzi mkuu wa Machi 4.
Madai hayo kutoka muungano wa CORD, wenye chama cha ODM kinachoongozwa na Waziri Mkuu, yameibua hisia kali kwa wanasiasa na hata wasiohusika na siasa.
Japo sio Waziri Mkuu Raila Odinga aliyetoa madai hayo, bwana Uhuru Kenyatta aliyekuwa huko Pwani mwishoni mwa wiki kuendesha kamepni za kisiasa, ameyajibu madai hayo moja kwa moja.
Mshirika wake Raila Odinga, bwana Franklin Bett ambaye anaongoza bodi ya uchaguzi katika chama cha ODM, ndiye aliyeibua madai hayo, akiwalaumu maafisa fulani serikalini.
Mjini Mombasa kuna malumbano kama hayo, na ofisa wa tume ya uchaguzi IEBC kaunti ya Mombasa, Laban Mwadime amewaonya wanasiasa dhidi ya kukiuka taratibu zinazoambatana na uchaguzi.
Wakati huo huo tume ya uchaguzi inaendelea kuwahamasisha wapiga kura ikiwa takriban wiki mbili kabla ya uchaguzi mkuu wa Kenya kufanyika.
0 comments:
Post a Comment