BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

LEMA APATA DHAMANA, ATIKISA JIJI LA ARUSHA.

Kwa ufupi
Mara baada ya kuwasili, Lema alipelekwa moja kwa moja, katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi, Devota Msofe ambacho kilikuwa kimejaa idadi kubwa ya maofisa wa polisi na wananchi wengine.http://www.mwananchi.co.tzMbunge wa Arusha Mjini,Godbless,Mbunge wa Arumeru Mashariki na wafuasi wa Chadema wakitoka  kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi baada ya  Mbunge wa Arusha Mjini,Godbless Lema kusomewa mashtaka ya uchochezi katika Chuo cha Uhasibu  Arusha(IAA) wiki iliyopita na kusababisha wanafunzi kumzomea Mkuu wa Mkoa,Magesa Mulongo.Picha na Filbert Rweyemamu.

ARUSHA. 
SHUGHULIZA mbalimbali katika Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha, jana zilisimama kwa muda asubuhi baada ya mamia ya watu kufurika kusikiliza kesi ya Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema (36).


Mbunge huyo alifikishwa mahakamani, saa 2:40 asubuhi akiwa kwenye gari dogo akisindikizwa na gari la askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) ambako alipokewa na mashabiki wake waliokuwa wakiimba nyimbo mbalimbali za kumsifia.


Idadi kubwa ya maofisa wa usalama na askari kanzu, haikuwatia hofu wafuasi wa mbunge huyo ambao walikuwa na mabango na majani, huku wakii
mba mbunge... mbunge..., Lema Jembe, hatumtaki Mkuu wa Mkoa na kuzua patashika aina yake mahakamani kati yao na askari.


Viongozi wa Chadema, wakiongozwa na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari na Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Aman Golugwa walifanya kazi ya ziada kuwatuliza wafuasi hao ili kuruhusu shughuli nyingine kuendelea lakini mara kadhaa walilipuka kwa kauli za ‘peoples power.’


Mara baada ya kuwasili, Lema alipelekwa moja kwa moja, katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi, Devota Msofe ambacho kilikuwa kimejaa idadi kubwa ya maofisa wa polisi na wananchi wengine.

Kesi yaanza
Hakimu Msofe aliingia katika chumba cha Mahakama saa 3:05 na kesi hiyo kuanza.

Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Eliainenyi Njiro, alisema Lema anashtakiwa kwa kosa la uchochezi katika Chuo cha Uhasibu, alilofanya Aprili mwaka huu ambalo alisema ni kinyume cha Kifungu cha 390, Kifungu kidogo cha 35 cha Sheria Sura ya 16 ya Makosa ya Jinai kama yalivyorekebishwa mwaka 2002.


Alinukuu maneno ya Uchochezi aliyosema Mbunge Lema kuwa ni:
“Mkuu wa Mkoa amekuja kama anakwenda kwenye Send Off, hajui Chuo cha Uhasibu kilipo, wala mauaji ya mwanafunzi wa chuo, ameshindwa kuwapa pole ya kufiwa na kusikiliza shida zenu na anasema hawezi kuongea na wanafunzi wasio na nidhamu.” Baada ya Lema, kusomewa mashtaka hayo, alikana.


Kuhusu dhamana, Njiro alisema upande wao hauna pingamizi ikiwa masharti yatakayotolewa na hakimu yatatekelezwa na aliomba kesi hiyo, kupangiwa siku nyingine ya kutajwa kwani bado upelelezi unaendelea.

Wakili wa Lema, Method Kimomogoro alisema mshtakiwa ni Mbunge hivyo anaweza kujidhamini kwani hawezi kukimbia popote duniani.

Alisema hata makosa ambayo anadaiwa kutenda hayajulikani uelekeo wake kama ni makosa. Mbali ya Kimomogoro, Lema pia anatetewa na Hamphrey Mtui.


Hakimu Msofe alitoa masharti ya dhamana akisema mshtakiwa atadhaminiwa na mtu mmoja ambaye atasaini fomu ya Sh1 milioni na awe na barua ya kumtambulisha na kitambulisho. 

Diwani wa Viti Maalumu (Chadema), Sabina Francis alimdhamini, hivyo Hakimu Msofe kutoa dhamana hadi Mei 29 kesi hiyo itakapotajwa tena.


Baada ya kuahirishwa kwa kesi hiyo, mamia ya wafuasi wa Chadema waliokuwa nje ya Mahakama, walilipuka kwa shangwe wakiimba na kuonyesha mabango yenye ujumbe mbalimbali na majani kuashiria amani.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: