BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RAIS WA SUDAN EL BASHIR KUWAACHIA WAFUNGWA WOTE WA KISIASA.

Rais Omar el Bashir.

RAIS wa Sudan Omar al Bashir, ameagiza kuachiliwa huru kwa wafungwa wote wa kisiasa.

Katika hotuba yake ya ufunguzi wa vikao vipya vya bunge, Rais Bashir alitoa wito wa kufanyika mashauriano na vyama vingine vya kisiasa.

Wiki jana makamu wa rais Ali Osman Taha aliwaalika waasi kutoka majimbo ya Kordofan Kusini na Blue Nile,kushauriana kuhusu katiba mpya.

Hata hivyo walikataa mwaliko huo.

Waandishi wa habari wanasema kuwa hali ya wasiwasi imeanza kupungua kati ya Sudan na Sudan Kusini tangu nchi hizo mbili zikubaliane kurejelea shughuli ya kuchimba na kusafirisha mafuta.
BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: