BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

DEREVA WA BODA BODA AGONGA TRENI MOROGORO.


 Wasamalia wema waliojitokeza eneo la tukio wakimkimbiza kijana huyo hospital.kijana huyo ambaye jina lake halikupatikana mara moja amenusurika kifo baada ya pikipiki yake kugongwa na Treni mkoani morogoro.endelea kupitia audifacejackson blog .Kijana huyo ambaye inadaiwa  alikuwa akimkimbizia chakula cha mgonjwa  aliyelazwa hospital ya rufaa ya mkoa wa Morogoro,alivunjika mguu wa kulia na kukimbizwa hospital hiyo ya mkoa wa Morogoro kwa matibabu


  Shuhuda wa tukio hilo Bw Athanas Kessy akizungumza na audifacejackson blog eneo la tukio amesema kwamba  haraka ya kijana huyo ndiyo iliyosababisha ajali hiyo.Mimi nilifika hapa na kuona kichwa tupu cha Treni kikipiga hodi nyingi kikiashiria watu kusimama baada ya kufika kwenye makutano haya ya barabara ya Mji Mpya chaajabu boda boda huyu alipofika eneo hili licha ya kusikia honi hizo  hakutaka kusimama na kuvuka fasta hata hivyo katika hali ya kushangaza alipoikanyaga reli  pikipiki yake ilikata moto na kuzimika akiwa katikati ya reli hiyo na kushuhudia akigongwa na kichwa hicho cha Tren dereva wa tren hiyo alipofika eneo la tukio nilimshuhudia akishika kichwa kwa uchungu lakini hakuwa na njia nyingine ya kumkwepa"alisema Bw Kessy


 Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo akianglia kwa masikitiko kofia nguo'Herment' aliokuwa amevaa kijana huyo,ambayo alipasuka vipande vipande.kama inavyoonekana pichani.audifacejackson blog inampa pole sana kijana huyo na kuwaasa vijana wengine hasa waendesha bodaboda kuwa watulivu barabarani na kufuata sheria za usalama barabarani kwa lengo la kuzuia ajali za mara kwa mara .


  Mashuhuda wengine wakiikagua pikipiki iliyogongwa na treni mapema leo asubuhi mjini morogoro.


   Baada ya kugongwa na Tren pikipiki hiyo ilirushwa mbali na eneo la tukio ikiwa imeharibika vibaya


 Askari wa kikosi cha usalama barabara mkoa wa Morogoro,baada ya kuwasili eneo la tukio walisalimiana  na diwani msaafuu wa kata ya Mji Mpya Bi Emmy Kiula ambaye tukio hilo limetokea jirani kabisa na nyumba yake na kwamba yeye ndiye aliyetoa taarifa polisi na kulinda vifaa vya dereva huyo wa boda boda,mama huyo pia ni muweka hazima wa tawi la yanga Safi la mkoani Morogoro ambapo ofisi za tawi hilo ziiko kwenye nyumba yake.,


          


endelea kupitia audifacejackson blog

 

Kwa sheria za nchini kijana huyo ndiye mwenye makosa kwa kuigonga treni hiyo.
Chanzo http://audifacejackson.blogspot.com
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: