Akiandaa kupanda mti.
Akipanda mti.
Katibu Mkuu wa wizara ya Maliasili na Utalii, Maimuna Tarishi akiwa katika matukio matatu tofauti wakati wa maadhimisho ya siku ya upandaji miti kitaifa iliyofanyika kando ya Bwawa la Mindu kata ya Magadu Manispaa ya Morogoro ambapo jumla ya miti 2300 ilipandwa katika eneo hilo mkoani Morogoro.
PICHA JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM
Makamu Mkuu wa chuo cha kilimo cha Sokoine Morogoro Profesa Gerald Monella naye akipanda mti wakati wa maadhimisho hayo.
Juma Mtanda, Meneja Blog akipanda mti katika maadhimisho hayo.
Mhifadhi wa misitu katika safu ya milima ya Uluguru, Sosteness Rwamungira naye akipanda mti.
Mwanafunzi wa chuo hicho akipanda mti.
Katibu Mkuu wa wizara ya Maliasili na Utalii, Maimuna Tarishiakihutubia wananchi katika kilele cha maadhimisho ya siku ya upandaji miti kitaifa iliyofanyika Morogoro April 3 mwaka huu.
Katibu Mkuu wa wizara ya Maliasili na Utalii, Maimuna Tarishi akiteta jambo na Makamu wa mkuu wa chuo cha kilimo cha Sokoine (SUA) Profesa Gerald Monella.
Sehemu ya maprofesa wa chuo cha kilimo cha Sokoine Morogoro (SUA) wakifuatilia matukio mbalimbali katika maadhimisho hayo.
Na
Juma Mtanda, Morogoro.
SERIKALI
imekuwa ikichukua hatua mbalimbali za kusimamia na kuhifadhi misitu ili iweze
kuchangia kikamilifu katika kuhifadhi mazingira kwa kutoa mazao na huduma
endelevu kukidhi mahitaji ya watanzania wote hususani katika kujiongezea kipato
na kuondoa umasikini.
Hayo
yalisemwa jana na Katibu mkuu wa Wizara ya maliasili na utalii Maimuna Tarishi
kwa niaba ya Waziri wa wizara hiyo Balozi Khamis Kgasheki wakati wa maadhimisho
ya siku ya taifa ya kupanda miti iliyofanyika kandokando ya bwawa la Mindu
lililopo katika kata ya Magadu Manispaa ya Morogoro.
Katibu
Mkuu huyo alisema kuwa baadhi ya hatua zilizochukuliwa na serikali katika
kuhifadhi misitu na kutunza mazingira ni pamoja na kuanzishwa na kwa wakala wa
huduma za misitu kwa madhumuni ya kuongeza ufanisi na tija katika kusimamia na
kuhifadhi rasilimali za misitu na nyuki nchini.
Alisema
kuwa takwimu za hivi karibuni zinaonesha kuwa miti inayotumika nchini ni meta
za ujazo milioni 87 kwa mwaka na kwamba matumizi hayo ni makubwa ukilinganisha
na ukuaji wa miti ambao ni meta za ujazo milioni 76 kwa mwaka.
Aidha
alisema kuwa tafiti zilizofanywa sehemu mbalimbali duniani zinaonesha kuwa
misitu inatoweka kwa kasi ya nusu kilometa ya mraba kila dakika sika na kwamba
iwapo mwenendo huo utaendelea ifikapo mwaka 2035 misitu minene yote duniani
ikiwa nia pamoja nay a Tanzania itakuwa imekwisha.
Naye
makamu mkuu wa chuo cha Sokoine Sua Profesa Gerald Monella alisema kuwa shughuli
za upandaji miti katika chuo hicho zimekuwa zikifanywa kila mwaka na ni moja ya
sehemu ya utekelezaji wa majukumu ya chuo hicho.
Profesa
Monella alisema kuwa shughuli za upandaji miti chuoni hapo unalenga katika
kuhifadhi ardhi na mazingira, kutunza mipaka ya chuo na shughuli za kitaaluma
ambapo katika kipindi hiki cha mwaka 2013-2014 chuo hicho kimepanga kupanda
miti 2300 ya mikenge katika maeneo mbalimbali ikiwemo kwenye bwawa la mindu.
0 comments:
Post a Comment