TESHA BAADA YA KUMWAGIWA TINDIKALI
-------------
Kada maarufu wa CHADEMA
Shinyanga mjini,Bwana Oscar Kaijage,Jumamosi alikamatwa na askari polisi
na kuzuiwa kituo cha kati na jana Jumatatu alisafirishwa kwenda Tabora
na kukabidhiwa kwa askari wa huko.
Sababu kuu ya kukamatwa,ni kuhusishwa na tukio la kumwagiwa tindikali Bwana Musa Tesha 9
Sept,2011 huko Igunga kwenye kampeni za uchaguzi mdogo wa Mbunge ambapo
mgombea wa CCM bwana Peter Kafumu alimshinda mgombea wa CHADEMA bwana
Joseph Kashinde.
Bwana Oscar alifuatwa dukani kwake stand ya mabasi ya Shinyanga mjini mnamo saa 9 mchana na askari nane ambao hawakuvaa sare.
Baada ya mazungumzo ya muda mfupi askari hao waliwaomba majirani wa duka hilo wasogee ili wawe mashuhuda wakati wanampekua.
Hata hivyo,polisi hao
hawakukuta kitu chochote walichokihitaji na kuamua kuondoka naye kwenda
kumpekua nyumbani kwake ambako nako pia hawakuambulia kitu.
Taarifa iliyopatikana jana mchana kutoka ofisi ya RPC shinyanga ni kuwa Oscar amepelekwa Tabora kwenda kufunguliwa mashitaka.
0 comments:
Post a Comment