Milipuko miwili mikubwa iliyotokea kwenye mstari wa mwisho wa kumalizia mbio za Boston Marathon umewauwa watu 3 nchini Marekani.
SHIRIKA la ujasusi la FBI nchini Marekani limesema
linachunguza kile inachodhania kuwa shambulio la kigaidi kufuatia
mashambulizi mawili ya mabomu mwishoni mwa mbio za marathon za Boston.
Milipuko hiyo miwili mikubwa iliyotokea kwenye mstari wa mwisho wa kumalizia mbio za Boston Marathon nchini Marekani imewauwa watu watatu na kuwajeruhi wengine zaidi ya mia moja.
Mlipuko wa pili ulitokea sekunde chache tu baada ya ule wa kwanza kutokea wakati mamia ya wanariadha wakikamilisha mbio zao huku wakishangiliwa na umati.
Waliojeruhiwa walikimbizwa hospitalini huku wengi wao wakitokwa na damu.
Rais Barack Obama amesisitiza kuwa serikali serikali itakahikisha kuwa washukiwa wa mashambulizi hayo lazima atakamatwa.
Picha na video kutoka Boston zilionyesha watu wakiwa wamechanganyikiwa wasijue pa kwenda, huku magari ya huduma za dharura yakielekea katika eneo la tukio na watu waliojeruhiwa vibaya wakipelekwa kwenye hema la matibabu ya haraka.
"Kuna watu wengi wamelala chini," alisema mwanariadha mmoja akinukuliwa na chombo cha habari cha AP.
Tukio hilo linaripotiwa kutokea saa tatu baada ya washindi kuvuka mstari wa ushindi.
"Kulikuwa na mlipuko, polisi, moto na EMS kwenye eneo la tukio. Hatuna namna ya kufahamu namna watu walivyojeruhiwa," msemaji wa Polisi Boston alisema.
Shirika la habari la AP linasema kulikuwa na sauti kubwa ya mlipuko upande wa kaskazini mwa mtaa wa Boylston Street, karibu tu daraja linaashiria mstari wa kumalizia mashindano. Mlipuko mwingine ukasikika dakika chache baadaye.
Mike Mitchell wa Vancouver kutoka Canada, mwanariadha aliyemaliza kukimbia alisema alikuwa akiangalia nyuma ya mstari wa kumalizia mashindano ndipo aliposikia ‘mlipuko mkubwa’
Inataarifiwa kuwa moshi ulipanda juu hewani kiasi cha futi 50 (mita 15),' aliliambia shirika la habari la Reuters , na watu wakaanza kukimbia wakipiga mayowe baada ya kusikia.
Waliokuwa wakimalizia mbio hizo waliongozwa kuepuka eneo lenye moshi kwenye mlipuko wakati huo huo eneo hilo likifungwa.
Tawi la Msalaba Mwekundu la Mashariki mwa Massachusetts limetenga kituo cha kusaidia majeruhi.
0 comments:
Post a Comment