BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KUFANYA VIBAYA KWA SIMBA SC LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA KWACHANGIWA NA MAKUNDI.

Mashabiki wa klabu ya Simba SC tawi la Mpira na Maendeleo makao makuu jijini Dar es Salaam wakinunua samaki eneo la Msamvu Manispaa ya Morogoro wakati wakitokea jijini Mwanza ambako timu yao ilicheza na Toto Afrika katika mchezo wa ligi kuu ya vodacom Tanzania bara na kutoa sare ya bao 2-2.

Na Juma Mtanda, Morogoro.
KUFANYA vibaya kwa klabu ya Simba SC katika ligi kuu ya vodacom Tanzania bara na kutolewa katika ligi ya mabingwa Afrika kumedaiwa kuchangiwa na baadhi ya makundi kutumiwa na baadhi ya viongozi kutaka madaraka yaliyopelekea kumpindua mwenyekiti wa klabu hiyo.

Akizungumza na gazeti hili mjini hapa Afisa Habari wa tawi la Simba SC mpira na Maendeleo makao makuu jijini Dar es Salaam, Jackson Tollo alisema kuwa kufanya vibaya kwa klabu hiyo ligi kuu ya vodacom Tanzania bara na kutolewa mapema katika ligi ya mabingwa Afrika kumetokana na kuwepo kwa migogoro ndani ya klabu hiyo iliyozalishwa na kundi la Mpira Pesa kwa madai kuwa mwenyekiti Ismail Aden Rage ameshindwa kuiongoza Simba.

Tollo alisema kuwa kundi la Mpira Pesa ndilo linalodaiwa kuchochea kwa Simba kufanya vibaya katika ligi hiyo hasa kwa baadhi ya viongozi kutaka nafasi ya uenyekiti kwa kupitia migogoro inayoratibiwa na kundi la Mpira Pesa na kudaiwa kuwashawishi baadhi ya wachezaji kucheza chini ya kiwango na kupata matokeo mabaya.

Baadhi ya viongozi ndani ya Simba SC wanataka nafasi ya uenyekiti kwa kuanzisha migogoro kupitia kundi hilo la Mpira Pesa na kueleza kuwa mapinduzi yaliyofanyika hivi karibuni hayakuwa halali kwani hayakubarikiwa na makundi mengine jambo ambalo imeiyumbisha timu  katika mbio za kutetea ubingwa wa ligi kuu ya vodacom msimu huu.

“Ni kundi moja tu lenye maamuzi ndani ya Simba SC na hilo ni Mpira Pesa ilhali kuna makundi zaidi ya 80 na lengo la kuundwa kwa makundi hayo ni kuwapa hamasisa wachezaji wakati wa mchezo kwa kuwashangilia ili kuweza kupata ushindi. Alisema Tollo.

Wameitisha mkutano na kutangaza kumpindua mwenyekiti wa Simba kinyume na utaratibu na badala yake walipaswa kujadiliana na makundi yote ndani na Dar es Salaam ili kujadili mwenendo wa klabu hiyo jambo ambalo hawakulifanya.

Hakuna haja ya kumtafuta mchawi kwa Simba kufanya vibaya mchawi yupo kuwa ni tawi la Mpira Pesa ambalo ndilo linayumbisha wachezaji na kupelekea baadhi ya wachezaji hao kusimamsihwa kutokana na madai ya utovu wa nidhani ambao. Alisema Tollo.

Alitoa wito kwa makundi mengine kuendelea kutoa ushirikiano kwa uongozi uliopo madarakani na wachezaji ambao kwa sasa wanacheza kwa uelewano mkubwa ambao wameonyesha katika mchezo dhidi ya Toto Afrika ambapo yoso saba walianzaa katika kikosi cha kwanza.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: