BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

LIEWING: AZAM FC HAITOKI KWA CHIPUKIZI WANGU

Kwa ufupi

Kocha wa Simba, Patrick Liewig amewataka mashabiki wa klabu yake wasiwe na mashaka kwani chikukizi wake wana uwezo wa kuwaadabisha Azam hata Yanga.
http://www.mwananchi.co.tz
 KOCHA WA SIMBA PATRICK LIEWING
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiGvUqNEiLyqh7UFAG5RhyAuoJb95C2gFHS1vjExxVdDglZIz3hy49lb7IW_V0z_XMDiYvuh74teG25OIGW-VyJcFhx0PjICTV_sG8HNOxK7HLwgJWFhdx8E5dDGeM6SxCGOxoW3kPXCds-/s1600/Kikosi+cha+Simba.JPG
KIKOSI CHA SIMBA SC.
DAR ES SALAAM
KOCHA wa Simba, Patrick Liewig amewataka mashabiki wa klabu yake wasiwe na mashaka kwani chikukizi wake wana uwezo wa kuwaadabisha Azam hata Yanga.
Baadhi ya mashabiki wa Simba wamekuwa na mashaka na ubora wa kikosi chao kama kina uwezo wa kuzimudu Azam na Yanga na kupata matokeo mazuri kufuatia msimamo wa Liewig wa kuwatumia zaidi chipukizi badala ya wachezaji wakongwe.
Simba inayokamata nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu itashuka dimbani Aprili 13, kuvaana na Azam katika pambano litakalopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam huku ikitarajiwa kuikabili Yanga Mei 18.
Akizungumza na gazeti hili jijini Dar es Salaam jana, Liewig alisema haoni sababu ya mashabiki wa klabu hiyo kuwa na mashaka kwa sababu chipukizi wake wamepevuka vya kutosha na wana uwezo wa kuikabili timu yoyote kwenye ligi na kupata ushindi.
“Jana (Juzi) tulifanya mazoezi nikiwa na wachezaji 20 tu na wengi wao ni vijana, hakika wana hamu ya mafanikio, wanajituma na wana morali ya juu,” alisema Liewig.
Alisema “Mechi inayofuata tunacheza na Azam, naamini kwa kutumia kikosi hiki hiki matokeo mazuri yatapatikana, jambo la kufurahisha ni kwamba watashirikiana na wachache wenye uzoefu kama Juma Kaseja na Amri Kiemba ambao ni kama walimu kwao, hakuna sababu ya kuwa na mashaka,” alisema Liewig.
Alisema kuwa ataendelea na msimamo wa kuwatumia wachezaji vijana kwa vile ndiyo dira hasa ya Simba kufikia mafanikio.
Naye kocha wa Azam, Stewart Hall alisema mawazo yake kwa sasa ni juu ya mchezo wa Jumatano dhidi ya African Lyon na siyo Simba wala Yanga.
Hall alisema kwa kuzingatia hatua ligi ilipofikia hawezi kuipuuza Lyon badala yake atakiandaa kikosi chake kikamilifu kwa lengo la kuhakikisha kinavuna pointi tatu kwenye mchezo huo.
“Akili na nguvu zangu zote sasa nimezielekeza kwenye mchezo na African Lyon siku ya Jumatano na siyo hata kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, hauwezi kuwaza jambo la lililoko mbali wakati kuna lingine lipo karibu na unatakiwa kukabiliana nalo,” alisema Hall.
”African Lyon haiko katika wakati mzuri wakati huu, inapigana kwa ajili ya kuhakikisha inapata ushindi ikiwezekana iepuke kushuka daraja, ni mechi ngumu, ni lazima tujiandae kisawasawa.”
Katika pambano la kwanza lililopigwa Oktoba 6, mwaka jana, Azam iliizamisha Lyon bao 1-0.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: