BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

TP MAZEMBE YATOA DOZI KWA MOCHUDI CENTRE CHIEF YA BOSTWANA KWA KUITANDIKA BAO 6-0 LIGI YA MABINGWA AFRIKA.



News Photo: Congos TP Mazembe forward Mbwana Ally Samatta vies…Samatta moja ya heka heka uwanjani dhidi ya klabu yake ya TP MAZEMBE.
image

KLABU ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), imeitandika Mochudi Centre Chiefs ya Botswana katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kufuatia ushindi wa bao 6-0 kwenye Uwanja wa Stade du TP Mazembe mjini Lubumbashi.

Mazembe tayari imefuzu kwa ushindi wa jumla wa 7-0, kutokana na ushindi wa awali dhidi ya timu hiyo ya Botswana kushinda 1-0 katika mchezo wa ugenini huku bao pekee likifungwa na Mtanzania, Mbwana Samatta.

Mabao ya Mazembe jana yalifungwa na Rainfrod Kalaba dakika ya sita na 35, Tressor Mputu dakika ya 15 na 80, Samatta dakika ya 75 na Eric Nkulukuta dakika ya 90.

Mazembe sasa itamenyana na Orlando Pirates ya Afrika iliyoitoa Zanaco ya Zambia kwa jumla ya mabao 3-1. Ikishinda 1-0 ugenini na 2-1 nyumbani jana.

Mbali na Samatta, katika kikosi cha Mazembe kuna Mtanzania, mwingine, Thomas Ulimwengu ambao wote wanafanya vizuri kwa sasa na pia ni tegemeo la nchi yao katika kampeni za kwenda Brazil 2014.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: