Mama Shida Salum.
SHIDA Salum
ambaye ni mama mzazi wa mwanasiasa machachari ambaye ni Mbunge wa Kigoma
Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe amesema kuna watu wanataka kumuua.
Akizungumza na gazeti hili kwa njia
ya simu Jumamosi iliyopita, Shida alisema Aprili 19, mwaka huu, saa moja na
nusu katika Ghorofa la NSSF maeneo ya Tabata Bima, hawezi kuisahau kwa kuwa
ndiyo siku ambayo majambazi walimvamia wakiwa na bastola.
Akisimulia mkasa huo Shida alikuwa
na haya ya kusema:
“Majambazi hayo yaliyonivamia
siyajui lakini mmoja wao huwa namuona. Kabla hawajaja walinipigia simu
wakaniambia wana shida na mimi lakini hatuk
upanga namna ya kuonana.
Uwazi: Sasa walipofika nyumbani
kwako, uliwakaribishaje?
Shida: Walipofika walivamia na
kufanikiwa kuingia sebuleni.
Uwazi: Baada ya kuingia ikawaje ?.
Shida: Cha kwanza walichotaka ni
laptop (Kompyuta mpakato), flash na simu zangu.
Uwazi: Uliwapa ?.
Shida: Baada ya kutoa amri hiyo
niliwajibu kuwa kompyuta iko ofisini na simu niliwaambia ziko kwenye chaji.
Uwazi: Baada ya hapo ikawaje ?.
Shida: Mmoja wa majambazi hayo
alinionyesha bastola kuwa kama sijatii hayo wanayoniambia basi watanifanya kitu
kibaya, ndipo nikamuita kijana wangu aitwaye Mtana aende chumbani kuchukua
simu zangu niwape.
Uwazi: Ikawaje ?.
Shida: Niligundua kuwa Mtana
alikuwa anasikia amri zilizokuwa zikitolewa na majambazi hayo, hivyo alipiga
kelele kuomba msaada kwa wananchi.
Uwazi: Majambazi wakafanya nini ?.
Shida: Waliposikia kelele
walikimbilia nje, wakaingia ndani ya gari lao ambalo namba zake zisijui,
wakatoweka.
Uwazi: Pole sana.
Shida: Pamoja na purukushani hizo
namshukuru Mungu sana kwa kuwa hawakunidhuru na hawakufanikiwa kuchukua
chochote.
Uwazi lilitinga nyumbani kwa mama
huyo na kukuta ulinzi ukiwa umeimarishwa ambapo sasa kuna askari wenye bunduki.
Kwa mujibu wa chanzo chetu,
majambazi hayo yalifanikiwa kuingia ndani baada ya mlinzi aliyekuwepo zamu
kwenda kubadili nguo za kiraia ili avae za kiaskari.
“Tukio lilikuwa la haraka sana, wakati
askari huyo anatoka kwenye kibanda cha kubadilishia nguo ndipo na wale
majambazi walipokuwa wakitoka ndani na kuingia kwenye gari lao,” kilisema
chanzo.
Waandishi wetu walimtafuta kiongozi
wa walinzi wanaolinda nyumbani kwa mama huyo, aliyejitambulisha kwa jina moja
la Ngosha na alipoulizwa kuhusu sakata la kuvamiwa alikiri kulifahamu.
“Baada ya tukio lile tumeimarisha
ulinzi ili kuhakikisha usalama wa watu na mali zao. Sasa tumeweka askari wenye
bunduki na tunaamini tukio kama hilo halitajirudia,” alisema Ngosha.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi
wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, ACP Marietha Minagi alikiri kutokea kwa tukio
hilo.
“Nina taarifa ya tukio hilo na
tunaendelea na upelelezi kuwasaka majambazi hao, wananchi waondoe hofu.”
alisema Kamanda Minagi.
Chanzo global publisher.
0 comments:
Post a Comment