Kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma David Misime akielezea
ukamatwaji huo na kuonesha tunguli walizokuwa wanatumia.
JESHI la Polisi Mkoa wa Dodoma linawashikilia watu sita ambao
wanajihusisha na vitendo vya kishirikina kwa kujifanya wanaagua na kufichua
watu wachawi katika vijiji mbalimbali. Wanaenda mbali zaidi na kudai wanafichua
watu wachawi wanaozuia mvua isinyeshe katika maeneo mbalimbali hapa Dodoma.
Watuhumiwa hao hujulikana hapa Dodoma kwa jina maarufu LAMBALAMBA. Watuhumiwa
walikamatwa tarehe katika kijiji cha MBALAWALA.
0 comments:
Post a Comment