ogoro, Joel Bendera ili kuweza kumweleza kero mbalimbali zilizpo katika shule hiyo hii ilikuwa Mei 29/ 2013.
PICHA JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM
Mmoja wa wanafunzi akieleza jambo mbele ya viongozi waliofika kutafutia ufumbuzi wa kero hizo.
Gari la askari likiwa eneo la tukio wakati wakiwalinda wanafunzi hao huku wakimsubiri mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera.
Askari wa jeshi la polisi akiwa katika lindo la kuwalinda wanafunzi hao.
Na Monica Lyampawe,TBC Morogoro.
WANAFUNZI wa kidato cha kwanza hadi cha sita
katika shule ya sekondari Mzumbe iliyopo wilaya ya Mvomero wamelazimika kuandamana kwenda ofisi
ya mkuu wa mkoa wakishinikiza kuboreshewa huduma muhimu mkoani Morogoro.
Maboresha wanayodai kuboreshewa shuleni hapo ni
pamoja na miundombinu ya vyoo, kuondoa ubadhirifu, uongozi mbovu na kukomeshwa vitendo
vya lugha chafu zinazo tolewa na baadhi ya walimu.
Maandamano hayo yalizimwa na jeshi la polisi usiku wa manane (saa 8 usiku) baada
ya jeshi hilo kupata taarifa za maandamano hayo na kulazimika kuwazuia katika eneo la Sangasanga barabara kuu ya Iringa-Morogoro
wakati wakielekea kwa mkuu wa mkoa
wa Morogoro Joel Bendera.
Wananfunzi hao ambao wana vipaji maalum wanadai kuwa maandamano hayo yanatokea baada ya
kuvumilia kwa muda mrefu na hivyo wameamua kupaza sauti zao wakibainisha
matatizo lukuki yanayo wasibu ambayo yanaweza kushusha kiwango cha taaluma yao.
Mkuu wa shule ya sekondari Mzumbe, Dismas Njawa
ameelezea namna alivyoweza kutatua baadhi ya matatizo lakini hayakukidhi haja
za wanafunzi hao.
Katibu tawala Mkoa wa Morogoro Elia Ntandu
alilazimika kwenda kuzungumza na wanafunzi hao asubuhi na kuahidi kuyafanyia kazi yale
yatakayo wezekana.
Wanafunzi hawakuelewa, na ndipo Serikali
ilipoamua kuifunga shule ya Sekondari ya vipaji maalumu, Mzumbe kwa muda
usiofahamika na kuwapa wanafunzi siku mbili, kuanzia leo, kuondoka shuleni hapo.
0 comments:
Post a Comment