Chaomba radhi baada ya kutokea Google.
Chuo
Kikuu cha Wits cha nchini Afrika Kusini kilitayarisha tanzia ya kifo
cha rais mstaafu wa nchi hiyo, Nelson Mandela wakati bado yuko hai.
Tanzia hiyo ilitokea katika Google search kitu kilichowastua na
kuwashangaza wengi.
Chuo hicho kimeomba radhi kufuatia tukio hilo na kusema tanzia hiyo
imetokea Google kimakosa. Waliitayarisha ili iwe kwenye system zao za
ndani lakini haikutakiwa ionekane kwa umma.
Kimesema tanzia hiyo ilitakiwa isionekane bado na iwe kwenye mitandao yao ya ndani lakini tatizo.
Kwa
kifupi ni kwamba, hawaombi radhi kwa kuandika tanzia hiyo, bali kwa
tanzia hiyo kuonekana. Swali langu ni, kwanini wametayarisha tanzia
wakati mzee bado yuko hai? Tanzia sio kitu kinachochukua muda mrefu
kuandika kama kitabu. Sehemu kama ya Chuo Kikuu, yenye waadhishi mahiri
wengi, ingewachukua chini ya lisaa limoja kuandika tanzia ya nguvu kama
kifo kikitokea. Kwanini kuitayarisha kabla? Anyway, tanzia yenyewe hii
hapa chini.
About mtanda blog
Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
0 comments:
Post a Comment