SENZI ZA UHAI WAKEALEN PAMIC AKIONYESHA KIPAJI CHAKE KATIKA MCHEZO WA SOKA MUDA MFUPI KABLA YA KUANGUKA NA KUAGA DUNIA.BAADA YA KUANGUKA CHINI. Alen Pamic aliyelala, akipatiwa huduma ya kwanza na wachezaji wenzake katika moja ya mechi alizowahi kuzimia uwanjani hivi karibuni kutokana na matatizo ya moyo.
Alen Pamic
ZAGREB, Croatia.
Hivi karibuni, Pamic alipoteza fahamu
katika mechi ya ligi dhidi ya Lokomotiva iliyopigwa Februari, ambapo
licha ya matatizo yake hayo alisisitiza kuendelea kucheza soka, huku
madaktari wake wakimruhusu kufanya hivyo.
NYOTA wa soka la kulipwa raia wa Croatia, Alen Pamic ameanguka
uwanjani na kufariki dunia wakati wa mechi ndogo isiyo ya kimashindano, gazeti
la kila siku la Vecernji List limesema katika toleo lake mtandaoni la leo Jumamosi.
Taarifa hiyo imeripotiwa kwa ufupi, huku ikiwa haina maelezo
zaidi kuhusiana na kifo cha Pamic aliyekufa akiwa na umri wa miaka 23 tu.
Pamic, aliyekuwa akichezea klabu ya NK Istra 1961 katika
ligi ya daraja la juu zaidi nchini hapa, alikuwa na historia ya matatizo ya
moyo, ambayo yalimwangusha dimbani mara tatu kabla ya tukio hilo lililochukua
uhai wake.
Hivi karibuni, Pamic alipoteza fahamu katika mechi ya ligi
dhidi ya Lokomotiva iliyopigwa Februari, ambapo licha ya matatizo yake hayo
alisisitiza kuendelea kucheza soka, huku madaktari wake wakimruhusu kufanya
hivyo.
Pamic aliyekuwa kiungo mahiri dimbani, aliutumia msimu mmoja
wa 2010/11 kuchezea klabu ya Standard Liege ya Ligi Kuu ya Ubelgiji, lakini
klabu hiyo ikamtema muda mfupi baada ya kupata shambulio la moyo na kuzimia
akiwa mazoezini, gazeti la Vecernji limesema katika taarifa yake.
Pamic ni mtoto wa nyota wa zamani wa kimataifa wa Croatia, Igor
Pamic, ambaye kwa sasa anainoa klabu ya NK Istra 1961 aliyokuwa akiichezea
marehemu.
0 comments:
Post a Comment