Binti mmoja aliyekuwa katika pilikapilika za maandalizi ya sikukuu
ya Eid Kariakoo alikutwa na mkasa baada ya kibaka mmoja kutaka kumpora
begi lake la mkononi.
Binti
huyo hakuwa tayari kuachia begi lake kirahisi, kitendo ambaacho
kilimuudhi kibaka huyo na kumpelekea kumkata na kisu kiganjani binti
huyo na kumtishia asipige kelele kwa kuwa atamfanyia kitu mbaya.
Kwa ujasiri aliokuwa kuwa nao binti huyo alipiga kelele zilizopelekea
wasamaria wema katika eneo hilo kumsaidia na kumtia nguvuni kibaka huyo
eneo la Kariakoo kituo cha mabasi yaendayo Mbagala.
Hatimaye Polisi jamii wakisaidiana na Maaskari wa Usalama barabarani walifika eneo la tukio na kumtia nguvuni kibaka huyo.
Picha na Juma Omari.
About mtanda blog
Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
0 comments:
Post a Comment