MBUNGE WA KIGOMA KASKAZI AWAUMBUA KWEUPE FREEMAN MBOWE NA DK SLAA KATIKA MKUTANO WA HADHARA UWANJA WA MWANGA CENTRE MKOANI KIGOMA.
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, amejibu mashambulizi kwa viongozi wa Chadema, kutokana na kile alichosema wanazunguka na kusema maneno yasiyo ya ukweli.
Akihutubia maelfu ya wananchi waliokusanyika katika Uwanja wa Mwanga Centre, Kigoma mjini, alisema alichukua kadi ya uanachama wa Chadema mwaka 1993 wakati huo, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Wilbrod Slaa akiwa bado yuko CCM.
"Wakati hao wenye midomo mikubwa wanaoongea sasa, walipokuwa wamekumbatia watawala, nyinyi mlikuwa mnapigwa mabomu kutaka mageuzi, eti leo wao wapinzani zaidi kuliko sisi na ndiyo maana hatuwezi kuwaachia.
Hatuwezi kukubali, hatutoki, demokrasia ni mchakato na mwenzenu nimekuwa kwenye mchakato huu. Kadi yangu ya Chadema nimeichukulia kwenye uwanja huu, tarehe moja mwezi wa nne mwaka 1993, nikiwa na miaka 16, wakati nachukua kadi yangu, Katibu Mkuu wa chama changu alikuwa yuko CCM.
Akizungumza kile alichosema ni uongo unaosambazwa na viongozi wa juu wa chama hicho, Katibu Mkuu Dk Slaa na Mwenyekiti wake Mbowe waligawana maeneo Mbowe akaenda Kanda ya Ziwa na Dk Slaa Kanda ya Magharibi.
Alisema kwenye mikutano hiyo, Mbowe anasema kuwa endapo mbunge huyo atarudi yeye Mbowe atajiuzulu, suala alilosema linaonyesha kuwa tayari ameshafukuzwa bila hata utetezi wake kusikilizwa.
Alisema baada ya viongozi hao kuzungumza na kusema mambo hayo na yeye aliamua kurudi nyumbani Kigoma na baada ya kuona hilo Dk Slaa akahoji mbunge huyo anafanya vikao hivyo kama nani.
"Mimi nimekata rufaa, wajumbe wa baraza kuu wa Mtwara, Ruvuma wanaandika barua wanataka mkutano mkuu, Katibu Mkuu akiwa Igunga anasema hiyo ni haramu na hao wafuasi wa Zitto watafanya Zitto afukuzwe, si __wamwamesha nifukuza? takachokuja kunijadili, hivyo si wameshanifukuza ? .
0 comments:
Post a Comment